KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KUDHAMINI MICHUANO YA GOFU YA WAITARA
Katibu
wa klabu ya Gofu ya Lugalo Kanali Mstaafu John Nyalusi akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es
Salaam juu ya mashindano ya siku moja ya gofu ya kumuenzi Mkuu wa
Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara yatakayofanyika katika klabu ya
Gofu ya Lugalo jumamosi hii. Kulia ni Meneja chapa (vileo vikali) wa
Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija ambao wanahusika na udhamini
wa utoaji tuzo, vinywaji na burudani katika kipindi chote cha
mashindano.
Meneja
chapa (vileo kali) wa Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija,
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani)
jijini Dar es Salaam kuhusiana na mashindano ya siku moja ya gofu ya
kumuenzi Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara yatakayofanyika
katika klabu ya Gofu ya Lugalo jumamosi. Kushoto ni katibu wa klabu ya
Gofu ya Lugalo Kanali Mstaafu John Nyalusi. Kampuni ya bia ya Serengeti
kupitia kinywaji chake kikali cha Johnnie Walker kitadhamini mashindano
na kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa mchuano huo.
Mabalozi
wa pombe kali ya Scotch Whisky “Johnnie Walker” wakionyesha aina
mbalimbali za chapa za pombe hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari juu ya mashindano ya gofu ya waitara ambayo yanatarajiwa kuanza
rasmi siku ya jumamosi katika viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia pombe hiyo kali ndio wadhamini wa
mashindano hayo ambapo pia watahusika na utoaji tuzo, vinywaji na
burudani katika kipindi chote cha mashindano.
KAMPUNI
ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia pombe yake kali ya Johnnie Walker
imetangaza rasmi udhamini wa mashindano ya gofu ya Waitara ambayo
yanatarajiwa kuanza siku ya jumamosi katika viwanja vya jeshi Lugalo
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika viwanja hivyo, Meneja Chapa wa pombe wa
Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Bw. Shomari Shija alisema kuwa
udhamini wa mchezo huu wa gofu ni kuhakikisha kuwa unaweza kuendelea na
kusifika kama michezo mingine ikiwa pia kama moja ya sehemu ya kurudisha
fadhila kwa jamii inayotuzunguka.
“SBL
inadhamini michuano hii kwa kipindi cha miaka mitano sasa na itajikita
hasa katika udhamini wa utoaji wa tuzo, vinywaji na burudani katika
kipindi chote cha mashindano”…alisema Bw. Shomari.
Naye
katibu wa michuano hiyo ya gofu Kanali mstaafu John Nyalusi aliishukuru
SBL kwa kuendelea kusaidia maendeleo ya mchezo huo na kuyaomba makampuni
mengine kujitokeza na kuunga mkono jitihada hizo za kuinua mchezo wa
gofu nchini.
“SBL
imekuwa katika mstari wa mbele katika kuuendeleza mchezo wa gofu nchini.
Ni moja kati ya wadhamini wetu wa kudumu kwa sasa…hivyo tunawashukuru
sana… tunaomba makampuni mengine zaidi yajitokeze kuunga mkono jitihada
hizi,” alisema Kanali Nyalusi.
Aliongeza
kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufunguliwa na jaji mstaafu Ndugu
Mark Bomani siku ya jumamosi saa nne asubuhi na kuwa mpaka sasa mwitikio
umekua mkubwa na tayari wachezaji 150 wameahidi kushiriki mashindano
hayo kutoka vilabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wenyeji wa Lugalo Golf
club, Dar es salaam Gymkhana club, Morogoro Gymkhana club, Arusha n.k.
Mashindano
ya gofu ya Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara huandaliwa
na kufanyika kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wake wa
kimichezo nchini kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club. Uwanja
wa gofu wa Lugalo ulianzishwa mwaka 2006 kwa mchango mkubwa uliotolewa
na Generali mstaafu George Waitara kipindi alichokuwapo madarakani, pia
kuendelezwa na Mkuu wa Majeshi aliyefuata na aliyeko madarakani kwa sasa
Generali Davis Mwamunyange.
No comments:
Post a Comment