DKT KIGWANGALLA ATOA USHAURI WAKE JUU YA UDHIBITI WA MADAWA SERIKALINI
Dkt Hamisi Kigwangalla Mbunge Mteule Nzega Vijijini CCM. |
MBUNGE
mteule jimbo la Nzega vijijini Dkt Hamisi Kigwangalla (CCM) ametoa
ushauri kwa wizara husika juu ya udhibiti wa kuvuja kwa madawa
serikalini na kwenda kwenye maduka binafsi.
Kupitia ukarasa wake facebook Kigwangalla amesema #Sasa Kazi Tu Changamoto
ya Udhibiti wa Kuvuja Madawa Kutoka Mfumo wa Serikali Kwenda Kwenye
Maduka ya Watu Binafsi ni Katika Mambo ambayo mgombea Urais wa CCM, Ndg.
John Pombe Magufuli alionesha kuwa yanamkera sana. Hivyo wananchi
wanasubiri kuona nini kitafanyika kutatua changamoto hii...kuna
'expectation gap' ambayo ni lazima izibwe ndipo watu wasadiki
kushuhudia #MabadilikoYaKweli.
Nimesikia
kuna mkakati wa kutaka kuondoa maduka yote jirani na hospitali za
serikali. Si wazo baya sana lakini ninaamini na ninajua kwa hakika
kabisa kuwa kuna suluhisho bora zaidi ya hilo.
Inawashangaza
watu wengi kuwa kwenye pharmacy za watu binafsi nje tu ya hospitali
kuna dawa za kutosha za kila aina wakati kwenye pharmacy ya serikali
ndani ya hospitali hakuna! Kuna watalamu wetu wanadhani suluhisho ni
kuzuia uwepo wa pharmacy karibu zaidi na hospitali.
Ninafahamu
kwa mfano, kuna tafiti zimefanyika pale Muhimbili kuhusiana na idadi ya
dawa zilizopo ukilinganisha na pharmacy mojawapo pale nje; matokeo ya
utafiti huo yakawa, Muhimbili kuna dawa tofauti tofauti 850 (lines),
wakati kwenye hiyo pharmacy kuna dawa tofauti tofauti takriban 3200!.
Unaweza
kusema si busara kuziondoa pharmacy hizi wakati tunajua kabisa kwenye
hospitali yetu pale hakuna dawa za kutosha, maana itakuwa ni usumbufu
kwa wagonjwa wanaoagizwa kutafuta dawa fulani ambayo Muhimbili haipo.
Unaweza kusema kuwa aina mbalimbali zaidi ya 2300 za madawa zimeibiwa
kutoka Muhimbili, na mimi hapo utanipa shida sana kukuelewa. Na
nitakuuliza, zimepitia wapi pamoja na ulinzi uliopo? Na kama ziliwahi
kuweza kutoka nje ya hospitali mpaka pharmacy, kwani pharmacy hiyo
ikihamia Kariakoo ama Posta kutakuwa kuna ugumu gani wa 'wezi' hao wa
madawa kuzifikisha huko pia kama wameweza kuzitoa?
Nadhani njia hii ni too 'mechanical' na haitoondoa tatizo zaidi ya kuzalisha tatizo lingine 'la usumbufu kwa wagonjwa'.
No comments:
Post a Comment