Timu ya Zanzibar Diaspora USA Yanyakua Kombe la Muungano Washington DC, Kwa Ushindi wa Mabao 7-1 dhidhi ya Tanganyika
Katika
shamrashamra za kusherehekea Miaka 51 kuungana Tanganyika na Zanzibar
na kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Timu ya Zanzibar Diaspora
nchini Marekani imeifunga bao 7-1 jirani zake timu ya Tanganyika USA.
Kocha wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir pamoja na Kapteni Deddy Rouba wakikabidhiwa Kombe la Muungano.
Mechi
hiyo ambayo imehudhuriwa na mgeni rasmi rais mstafu wa awamu ya pili wa
Tanzania Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi. ilifanyika katika viwanya
vilivyopo Walker Mill Road District Heights Maryland, ambapo pia
ilihudhuriwa na balozi wa Tanzania nchini Marekan Mhe. Liberata
Mulamula.
Mechi hizo hufanyika kila mwaka kwaajili ya kusherehekea kuungana kati ya Tanganyika na Zanzibar April 26, 1964.
Rais mstafu wa awamu ya pili wa Tanzania Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi baada ya kusalimiana na wachezaji wa timu zote mbili
Mapema Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi aliwataka waTanzania kuungana kwa pamoja bila ya kujali tafauti zao.Wakati
huo huo kabla ya mechi kuaza Alhajji Ali Hassan Mwinyi alisalimiana na
timu zote mbili na kuupiga mpira kuashiria kuaza kwa mechi hiyo.
Kikosi kamili cha timu ya Zanzibar Diaspora
Mashindao
hayo ambayo yaliwapa ushindi mnono Timu ya Zanzibar Heroes baada ya
kichapo cha 7-1 dhidi ya Timu ya Tanganyika katika mechi ya kutafuta
Bingwa wa Kombe la Muungano, bao la kwanza kwa timu ya Zanzibar
lilifungwa kwa njia ya Penalti mfungaji wa bao hilo alikuwa Yahya Kheri
na magoli mawili ya lifungwa na Wingi machachari Abdulla J. Somania,
mbao hadi timu kipindi cha kwanza kumalizika Timu ya Tanganyika
ilifungwa 3-0
No comments:
Post a Comment