Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd). Uteuzi huo wa
Dkt. Ben Moshi ni wa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 1
Machi, 2014.
Kutokana na uteuzi huo Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.) amewateua
wafuatao, kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya PUMA Energy
(T) Ltd kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 1 Machi, 2014:
Mhandisi Dkt. Malima MP. Bundara,
Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha GARETRACE;
Bw. Solomon R.M. Odunga; Katibu Mkuu Mstaafu;
Bw. James Andilile, Kamishna Msaidizi wa Nishati katika Wizara ya Nishati na Madini
Bw. Daniel N. Nsanzugwanko, Mtaalam Mshauri wa masuala ya biashara.
Imetolewa na
KATIBU MKUU
No comments:
Post a Comment