Wizara ya Ulinzi ya Tanzania yasaini Mkataba wa Makubaliano na Serikali ya Israel
Mkuu
wa Tawi la Usalama na Utambuzi Jeshini Brigedia Jenerali, Nicodemus
Elias Mwangela pamoja na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
kwenye masuala ya Ulinzi katika Wizara ya Ulinzi ya Israel, Brigedia
Jenerali Mstaafu, Michael Ben-Baruch wakiwekeana saini katika Mkataba wa
Makubaliano ya pamoja ya Ulinzi kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa la Tanzania na Wizara ya Ulinzi ya Taifa la Israel, tukio
hilo limehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la
Tanzania, Mhe. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi Dkt.
Florens Turuka, Balozi wa Israel nchini Kenya awakilisha pia Tanzania,
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Suleiman Salehe
pamoja na viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania.Tukio hilo
limefanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao Makuu ya Jeshi
Brigedia
Jenerali Nicodemus Elias Mwangela (kulia) pamoja na Brigedia Jenarali
Mstaafu Michael Ben-Baruch wakibadilishana mikataba hiyo mara baada ya
kumaliza zoezi la kuwekeana saini.
Brigedia
Jenerali Nicodemus Elias Mwangela akimkabidhi Brigedia Jenerali Michael
Ben- Baruch zawadi ya Nembo ya Jeshi la Kujenga Taifa la JWTZ
Brigedia
Jenerali Nicodemus Elias Mwangela (wa sita kulia) pamoja na Brigedia
Jenerali Mstaafu, Michael Ben- Baruch (wa saba kutoka kushoto), wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na
Israel pamoja na Balozi wa Israel nchini Kenya ambaye anawakilisha
Tanzania.
No comments:
Post a Comment