KAMPUNI YA ORYX GAS YAJIVUNIA KUWA RAFIKI WA MAZINGIRA
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
KAMPUNI
ya mama katika usambazaji na uuzaji wa gesi ya ORYX nchini ijulikanayo
kama ORYX ENERGIES LTD imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na
Serikali ili kuhakikisha nishati mbadala inatumika badala ya mkaa ambao
umeonekana kuwa wa gharama sana.
Akizungumza
katika kuadhimisha Wiki ya mazingira leo viwanja vya Mnazi mmoja jijini
Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mauzo kampuni ya gesi ya ORYX Jeffrey
Nasser amesema kuwa ORYX GAS amekuwa rafiki mkubwa wa mazingira pale
walipoamua kuletea nishati mbadala ya ges.
"Na
haikuishia hapo tu bali tuliwawezesha wananchi wengi sana nchi nzima
kuipata kwa gharama ndogo na hata yale maeneo ya wananchi wa hali ya
chini tumewawezesha kupata gesi yetu. Na Tunaamini tumeokoa miti mingi
ambayo ingekatwa kwa matumizi ya kupikia,"amesema.
Amefafanua
kwa ORYX GAS kwa nyakati tofauti wamekuwa wadau muhimu katika kuunga
mkono jitihada za Serikali katika kutunza mazingira, na kwa muda mrefu
wamekuwa na kampeni yao ya ORYX GAS "Rafiki wa Mazingira".
Hivyo
amesema katika kuadhimisha Wiki ya mazingira wameamua kuchukua fursa
kujiunga na wadau wengine kushirikiana katika kuelimisha wananchi
umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya
kupikia kwa gharama nafuu sana ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo
inachochea uharibifu wa miti na mazingira kwa ujumla.
"Lengo
letu ni kuhakikisha watu wote wanatumia nishati ya gesi, kampuni ya
ORYX imewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye maghara ya uhifadhi na mitambo
ya kujaza gesi nchi nzima.Hatutarajii kusikia tena uhaba wa gesi ya
kupikia nchini na hatutarajii kabisa watumiaji wa gesi wanarejea kwenye
mkaa na kuni kwa kukosa nishati hii ya gesi hapa nchini,"amesema.
Pia
Jeffrey amesema kuwa Mkaa ni gharama hasa kwa wakazi wa mijini na
kuongeza hivi sasa gunia la mkaa kwa wakazi wa Dar es salam limefikia
Sh.70,000 na wengi wanalalamika kuwa mkaa haumalizi mwezi.
"Sisi
tunawapa mtungi wa gesi wa kilo 15 ambao kwa familia ya watu saba
wanaotumia gesi pekee huweza kutumia kati ya siku 30 hadi 40. Mbali na
faida za gharama ndogo,gesi yetu pia ni salama kwa afya ya mtumiaji na
usafi wa mazingira ambapo tusingeanza usambazaji mkubwa wananchi
wangepaswa kuweka bajeti nyingine za matibabu ya madhara ya moshi
mwilini na ukarabati wa nyumba ambazo huchafuka sana kutokana na
matumizi ya kuni na mkaa,"amesema
Amesema kampuni yao ya ORYX imetoa shukurani kwa wananchi kwa muitikio mkubwa wa matumizi ya gesi kila siku inayoenda. "Muitikio
mkubwa umeonekana hasa pale ongezeko la watumiaji wengi wapya nchi
nzima wakinunua mitungi mipya ya gesi ya ORYX kwa matumizi
yao,"amefafanua.
Mkuu
wa Kitengo cha Mauzo ORYX GAS,Jeffrey Nasser akizungumza na waandishi
wa habari(hawapo pichani) juu yakuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza
mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama
nafuu ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa
miti na mazingira.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kulia) akimzikiliza
Menejacha wa Maendeleo ya Biashara Oryx Gas,Mohamed Mohamed ambabo
akifafanua juu ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira
kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu
ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na
mazingira,leo jijini Dar as Salaam katika kilele cha maadhimosho ya wiki
ya mazingira Duniani.
No comments:
Post a Comment