Halotel yazindua laini mpya za watu mashuhuri (VIP).
-Ni laini zenye gharama nafuu Zaidi, hazihitaji kujiunga kifurushi
Kampuni
ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imezindua laini
mpya za watu mashuhuri zilizopewa jina la VIP zitakazo wawezesha wateja
wa mtandao huo kufanya mawasiliano kwa makato ya gharama nafuu zaidi kwa
kila dakika na MB za intaneti watakazo tumia.
Laini
hizo za VIP zitawawezesha wateja wa mtandao wa Halotel nchi nzima
kuweza kupiga simu au kutumia intanenti kwa gharama nafuu kwa kutumia
salio la muda wa kawaida wa maongezi bila kuwa na ulazima wa kujiunga na
kifurushi chochote.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa
Kampuni hiyo, Mhina Semwenda, amesema kuwa, uzinduzi huo wa laini za VIP
ni mwendelezo wa ubunifu na maboresho ya huduma za mawasiliano kwa
wateja wa Halotel kwa kuwaokolea muda na gharama ambapo badala ya mteja
kutumia muda na gharama kujiunga na vifurushi vya kupiga simu kwa
mtandao wa Halotel na mitandao yote au vifurushi vya intaneti mteja
ataweza kutumia salio la muda wa maongezi kupiga simu au kutumia
intaneti bila kuhofia matumizi makubwa ya makato kwa gharama nafuu
zaidi.
“Huduma
hii inawalenga wateja wa vipato vya aina zote, wale wenye matumizi ya
kati, na matumizi makubwa, ambapo katika laini hii ya VIP makundi hayo
yamegawanywa kwa kupewa majina ambayo ni Silver kwa wateja wenye
matumizi madogo, Gold kwa wateja wa matumizi ya kati na Diamond kwa
wateja wa matumizi makubwa. Makundi haya yana lengo la kukidhi mahitaji
ya kila mteja kulingana na kundi alilomo.” Alisema Semwenda na kuongeza.
“Mfano
kwa mteja atakayenunua laini ya VIP ya Silver yenye thamani ya shilingi
elfu tano (5,000) kwa pesa hiyohiyo anaweza kupiga simu Halotel kwenda
Halotel kwa gharama ya makato ya shilingi thelathini (30) tu kwa dakika
ambapo kwa makato ya gharama ya kawaida ni shilingi (228) kwa dakika
ambapo ni mara punguxo la mara saba(7) ya gharama za kawaida.
Vile
vile mteja katika kundi hili anaweza kupiga simu kwenda mitandao yote
kwa gharama ya makato ya shilingi arobaini na tano (45) tu kwa dakika
tofauti na makato ya gharama ya kawaida ambayo ni shilingi (228) kwa
dakika ambapo ni punguzo mara tano (5) ya gharama za kawada. Kwa MB 1
mteja atatumia intanenti kwa gharama ya shilingi nne (4) tu akiwa na
laini ya Silver ya VIP gharama ambayo ni mara saba(7) pungufu ya makato
ya gharama ya kawaida ya shilingi 30.72 kwa MB huku akifurahia kutumia
Facebook bure.” Alisema Semwenda.
Mteja
yeyote wa Halotel wa kawaida ana uhuru wa kuweza kubadili laini yake na
kuwa laini ya VIP na kuweza kufurahia kupiga simu Halotel na mitandao
yote pamoja nakutumia Mb za intanenti kwa kupiga *148*66# kisha
anachagua namba tisa (9) na hivyo kuendelea kuchagua kundi atakalohitaji
kujiunga, si hivyo tu mteja wa Halotel wa kawaida anaweza kuendelea
kujiunga na vifurushi kama kawaida endapo atahitaji.
Hii ni
moja ya maendeleo ya teknolojia katika kuendelea kuboresha huduma kwa
wateja wetu ambao wamekuwa na imani kubwa ya huduma zetu siku zote”
alisema Tito.
“Tunatarajia
huduma hii ya VIP itaongeza nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja
wetu na kwa watanzania wote, na kuokoa kiasi kikubwa cha gharama za
mawasiliano zinazokatwa wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi na wateja
wengine walioko sekta zingine mijini na vijijini ambako maeneo haya kwa
kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kuwasiliana,
biashara na kupata taarifa mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii kwa
kutumia intaneti kwa uhakika. Alihitimisha Semwenda.”
Meneja
wa idara ya ushirika Halotel Emmanuel Tito Malyeta, Halotel akiwaeleza
waandishi wa Habari, akitoa ufafanuzi mbele ya waandish wa Habari katika
uzinduzi wa huduma ya VIP ambapo Mteja yeyote wa Halotel wa kawaida ana
uhuru wa kuweza kubadili laini yake na kuwa laini ya VIP na kuweza
kufurahia huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu. Kushoto ni Meneja wa
Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel akiwaeleza waandishi
wa Habari, akitoa ufafanuzi mbele ya waandish wa Habari katika uzinduzi
wa huduma ya VIP, ambayo ni mwendelezo wa ubunifu na maboresho ya huduma
za mawasiliano kwa wateja wa Halotel kwa kuwaokolea muda na gharama
katika matumizi yao ya kila siku. Kulia ni Meneja wa idara ya ushirika
Halotel Emmanuel Tito Malyeta.
No comments:
Post a Comment