Header Ads

WANAFUNZI 78 WATUNUKIWA TUZO YA BALOZI WA CHINA KWA KUHITIMU LUGHA YA KICHINA, WIZARA YATOA NENO


 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia utoaji Tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania kwa wanafunzi ambao wamehitimu mafunzo ya Lugha ya Kichina
 Political Conceller wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Yang Tong (kushoto)akiwa ameshika tuzo pamoja na mwanafunzi baada ya kumkabidhi
 Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bao Bao Mariam Said akiwa ameshika tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania baada ya kutunukiwa jijini Dar es Salaam kutokana na kuhitimu mafunzo ya lugha ya Kichina ambayo yameandaliwa na Chama cha Kukuza Uhusiano Tanzania na China
 Baadhi ya raia wa China nchini Tanzania wakiwa wamebeba baadhi tuzo ambazo wametunukiwa wanafunzi waliohitimu kujifunza somo la Kichina
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Dk.Ave Maria Semakafu(aliyevaa gauni)akimkabidhi tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke mwanafunzi  wa Shule ya Nsingi Msoga Arafa Shaibu ambaye amehitimu lugha ya Kichina

 Mgeni rasmi katika utoaji wa Tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang  ambao wamehitimu mafunzo ya lugha ya Kichina,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Dk.Ave Maria Semakafu (wa kwanza mstari wa mbele)akifuatilia hotuba wakati wa utoaji Tuzo hizo
Political Counceller wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Yang Tong akizungumza kwa niaba ya Balozi wa nchi hiyo nchini Wang Ke wakati wa utoaji Tuzo kwa wanafunzi 78 wa Tanzania ambao wamehitimu mafunzo ya lugha ya  Kichina.Tuzo hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam.





Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JUMLA ya Wanafunzi 78 kutoka baadhi ya shule za msingi, sekondari na Vyuo Vikuu nchini wametunukiwa Tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke baada ya kuhitimu mafunzo ya lugha ya Kichina huku Wizara ya Elimu ,Sayansi, Teknolojia na Ufundi ikihimiza Watanzania kuchangamkia fursa kwa kujifunza lugha hiyo.

Mafunzo hayo ya lugha ya Kichina na mchakato wa utoaji tuzo hiyo ya Balozi wa China nchini yameandaliwa na Chama cha Kukuza Uhusiano wa China na Tanzania(Tanzania China friendship Promotion Association) ambacho Mwenyekiti wake ni Dk.Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu ni Joseph Kahama.

Akizungumza Dar es Salaam leo kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati wa utoaji tuzo hizo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Ave Maria Semakafu amesema kuhitimu kwa vijana hao 78 kwa kuifahamu lugha ya Kichina kutatoa fursa nyingi kwao ikiwamo ya kupata ajira katika nchi ya China kwani kuifahamu lugha yao ni sawa na kufahamu utamaduni wao.

Amefafanua kwa vijana wa Kitanzania ambao watakuwa wanakifamu vema Kichina ni rahisi kufundisha nchini China na kufanya kazi za aina mbalimbali pale watakapohitaji na kwa Tanzania kuna Shule 24 zinafundisha Kichina na wanafunzi wanaosoma somo hilo wanafanya mtihani.

Pia amesema kuna vijana wa Tanzania 4000 ambao wanasoma katika vyuo mbalimbali nchini China na kusisitiza kwa kukua mafunzo ya lugha ya Kichina yataendelea kutolewa ni vema vijana wakaendelea kuchangamkia fursa ya kujifunza lugha hiyo kama ambavyo raia wa China waliopo chini wanavyojifunza lugha yetu ya Kiswahili.

"Nitumie nafasi hii kumpongeza Balozi wa China nchini Tanzania kwa kuanzisha tuzo hii na taarifa ambayo tumepewa itakuwa ikitolewa kila mwaka baada ya watoto wetu ambao wanajifunza Kichina na kisha kufaulu mitihani ya lugha hiyo watakuwa wanatunukiwa.Hivyo ni jambo endelevu,"amesisitiza Dk.Semakafu.

Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke, Political Counceller wa ubalozi huo nchini Yang Tong amesema kutolewa kwa mafunzo ya Kichina kwa vijana wa kitanzania ni muendelezo wa kudumisha urafiki wa nchi hizo mbili ambao ni wa muda mrefu na umetokana na misingi mizuri iliyowekwa na waasisi wa nchi hizo miaka mingi iliyopita.

"Tanafahamu Tanzania inao marafiki wengi duniani lakini urafiki kati yake ya China una historia kubwa na hivyo tumeona ipo haja ya kufundisha lugha hiyo kama sehemu ya kuendelea kujenga uhusiano mzuri ambao umekuwa ukiendelea kuwa imara siku hadi siku,"amesema.

Kwa upande wa baadhi ya wanafunzi ambao wametunukiwa tuzo hiyo kwa kujifunza lugha ya Kichina akiwamo mwanafunzi wa Shule ya Msingi Msoga Arafa Shaibu na mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bao Bao Mariam Said wametoa mwito kwa wanafunzi wa shule mbalimbali kujifunza lugha hiyo wakiamini kuna fursa na faida nyingi ndani yake.

No comments:

Powered by Blogger.