MAKONDA APOKEA VIFAA VYA THAMANI MILIONI 400/- KWA AJILI YA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU
MKUU
wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhiwa vifaa vya ujenzi
vyenye thamani ya Sh.milioni 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel ltd
kwaajili ya kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam.
Vifaa
alivyokabidhiwa ni Mabati 15,000 yenye thamani ya Sh.million 360, nondo
tani 22 zenye thamani ya Sh.million 40 ambapo kiwanda hicho kimemuahidi
tena kumpatia vifaa vingine ikiwemo rangi, nondo na mabati.
Akipokea
vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam, Makonda ameshukuru kiwanda cha
MMI Steel chini ya Mkurugenzi wake Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa
kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu na kuwaomba wadau na wananchi
kujitokeza kuchangia kampeni hiyo ili kutoa heshima kwa walimu.
Aidha
amesema kampeni ya ujezi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo
hivi karibuni atapokea kontena nyingine 16 za furniture kutoka Marekani,
Kontena 10 za Vitabu kwaajili ya Maktaba ya jamii kutoka Marekani,
Kontena 10 za vifaa tiba kutoka Uingereza na kontena 10 za Maziwa kutoka
China kwaajili ya watoto waliojitokeza wakati wa mchakato wa kutafuta
haki ya watoto waliotelekeza kama sehemu ya msaada.
Kwa
upande wake Patel amesema wameamua kutoa vifaa hivyo kama sehemu ya
kutambua umuhimu wa elimu na kuunga mkono jitiada za RC Makonda katika
uboreahaji wa elimu kupitia mazingira bora ya walimu kufanya kazi.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kukabidhiwa vifaa mablimbali kwa ajili ujenzi wa
ofisi za Walimu na kiwanda cha MIN Steel vyenye thamani ya shilingi
milioni mia nne.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akiangalia mapati aliyo kabidhiwa
na kiwanda cha MMI Siteel kwajili ya kuezekea ofisi za walimu.
Mkuu
wamkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda(katikati) akimshukuru Mkurugenzi
wa Kiwanda cha MMI Steel Ltd,Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa
kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu (kulia) Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar
es salaam,Hamis Lissu.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).
No comments:
Post a Comment