BENKI YA STANBIC YABORESHA BIDHAA YAKE INAYOLENGA BIASHARA NDOGO NA ZA KATI
Kurahisisha huduma za kibenki kwa biashara ndogo na
za kati
Benki ya Stanbic Tanzania imeboresha
bidhaa yake ya kibunifu inayolenga wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) kwa
kuboresha ufanisi wa biashara zao. Benki hii sasa inatoa huduma bora za kibenki zilizo rahisi na zisizo
na usumbufu kupitia bidhaa yake ya Biashara Direct.
Katika taarifa iliyotolewa na
benki jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Farha Mohamed
alisema, "tunajivunia kuwapa Watanzania bidhaa yetu bora ya Biashara
Direct ambayo inarahisisha mchakato wa kibenki kupitia njia ya kidijitali kwa wafanyabiashara
wadogo na wa kati (SMEs), ikiambatana na msaada wa ushauri wa kifedha kwa wafanyabiashara
unaotolewa kupitia wabobezi wa biashara waliotengwa mahususi na benki.
Bidhaa yetu
sasa inaruhusu malipo kwa kutumia USSD kwa njia ya simu ya mkononi; ikiwa na chaguo
la lugha ya Kiswahili kuruhusu wateja wetu kuchagua lugha waipendayo.’’ Akichanganua
juu ya vipengele vya ulinzi na usalama wa bidhaa hiyo, Bi. Mohamed alielezea
kuwa malipo ya kupitia USSD yameboreshwa na kwa sasa, huduma hii ina uwezo wa
kunukuu na kuhakiki malipo. Muidhinishaji wa malipo anaweza kupokea nukuu ya
malipo haya popote alipo na kuweza kuyaidhinisha ili kukamilisha muamala.
Bidhaa hii mahususi kwa ajili
ya wafanyabiashara wadogo na wa kati imedhamiria kurahisisha uhamishaji wa
fedha, ulipaji wa bili pamoja na kuwawezesha wafanyabiashara hawa kufuatilia miamala
kwenye akaunti zao kirahisi - 'tunawezesha mafanikio ya kifedha kwa sekta ya
biashara ndogo ndogo na za kati (SME) kupitia Biashara Direct,' Farha aliongeza.
Nchi inapoelekea katika
msukumo wa maendeleo ya viwanda, ukuzaji wa sekta ya biashara ndogo na za kati
(SME) unaendelea kuwa nguzo muhimu katika kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo
ya Tanzania kufikia 2025. Kwa hivyo, Benki ya Stanbic imejitoa kufanikisha
maendeleo kwa wadau wanaojishughulisha katika biashara ndogo na za kati (SME)
kama ilivyodhihirika katika ushindi wake wa tuzo ya The Banker kama 'Benki bora
inayowezesha biashara ndogo ndogo na za kati (SME)’ nchini Tanzania iliotolewa hivi
karibuni.
No comments:
Post a Comment