MKUTANO WA KAMPENI MGOMBEA URAIS WA CCM ZANZIBAR DK SHEIN, VIWANJA VYA BUNGI ZANZIBAR
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia
Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi na Wana
CCM katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mpira
Bungu Wilaya ya Kati Unguja na kuomba Kura kuendelea kuiongoza Zanzibar
kwa Maendeleo katika sekta mbalimbali za Kijamii na kuendeleza kukuza
Uchumi wa Zanzibar.
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Mhe Shamsi Vuai Nahodha akiwahutubia Wananchi wakati wa
Mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika
viwanja vya mpira Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
Kada wa CCM Bi Amina Salum Ali akiwahutubia
Wananchi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar
kupitia CCM na kuwata kumpigia Kura ya Ndio Dk Ali Mohamed Shein, ili
kuendelea kuwaletea maendeleo. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla akiwahutubia Wananchi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpira Bungi Unguja.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla akiwahutubia Wananchi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpira Bungi Unguja.
Wanachama wa CCM wakiingia katika
viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali
Mohamed Shein, wakiwa na picha za Wagombea.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia
Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla alipowasili katika
viwanja vya Bungu kuendelea na Kampeni zake za kugombea Urais wa
Zanzibar kupitia CCM.
Mgombea Urais wa Zanzibar pia ni
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed
Shein, akiwasili katika viwanja vya bungi kuaza kwa kampeni yake akiwa
na Viongozi wa CCM kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai
Ali Vuai na kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan
Abdalla, wakielekea jukwaa kuu kwa ajili ya mkutano huo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini
Unguja alipowasili katika viwanja vya mpira bungu kuhudhuria Mkutano wa
Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi
wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed
Shein. uliofanyika katika viwanja vya bungi.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi
wakishangia wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar
kupitia CCM uliofanyika katika viwanja vya Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
Wanachama wa CCM wakimshangilia
Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein wakati akiwahutubia
katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vha mpira Bungi Wilaya ya
Kati Unguja.
No comments:
Post a Comment