Header Ads

Mkutano wa Kampeni Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Shein, Viwanja vya Bungi Zanzibar.

Wanachama wa CCM wakiingia katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakiwa na picha za Wagombea 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla alipowasili katika viwanja vya Bungu kuendelea na Kampeni zake za kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Mgombea Urais wa Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya bungi kuaza kwa kampeni yake akiwa na Viongozi wa CCM kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai na kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla, wakielekea jukwaa kuu kwa ajili ya mkutano huo. 
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar  kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein. uliofanyika katika viwanja vya bungi.

No comments:

Powered by Blogger.