CHINA NA TANZANIA ZAZINDUA UJENZI WA JENGO LA TAASISI YA MWALIMU NYERERE JIJINI DSM
Makamu
wa Rais wa China Li Yuanchao (wa pili kushoto) akiwa na mwenyeji wake
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati), akiwasili eneo
litakapojengwa jengo la Taasisi ya wa Mwalimu Nyerere karibu na bandari
jijini Dar es salaam. Makamu
wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (kulia) kwa pamoja wakizindua jiwe la msingi katika eneo
litakapojengwa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
salaam. Makamu
wa Rais wa China Li Yuanchao (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (wa pili kulia) kwa pamoja wakizindua wakimwaga mchanga
kuashiria kuanza kwa ujenzi jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini
Dar es salaam.Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing. Mama
Maria Nyerere (kushoto) akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya
tatu Benjamini Mkapa wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la
Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (kushoto)
akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye (kulia)
kuhusu picha ya mfano ya mwonekano wa jengo la Taasisi ya Mwalimu
Nyerere pindi litakapokamilika. Waziri
Mkuu mstaafu Frederick Sumaye akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya
tatu, Benjamini Mkapa (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya
(kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya
Mwalimu Nyerere (MNF). Makamu
wa Rais wa China Li Yuanchao (wa pili kushoto) akisalimiana na Mama
Maria Nyerere mara baada ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la
Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) jijini Dar es salaam wakishuhudiwa na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Makamu
wa Rais wa China Li Yuanchao ( kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, Mama Maria Nyerere, Rais
Mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya
tatu Benjamini Mkapa. Makamu
wa Rais wa China Li Yuanchao ( kushoto) akisalimiana na aliyekuwa Rais
wa Bunge la Afrika, Balozi Getrude Mongella wakati wa hafla ya uzinduzi
wa jingo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akisalimiana na Rais
mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Kulia) na Mama Maria Nyerere
wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria
uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Kutoka kushoto ni Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa Wawamu ya tatu,
Benjamini Mkapa,Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya na Waziri Mkuu mstaafu
Jaji Joseph Warioba.
No comments:
Post a Comment