Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe
Ramadhan Semtawa wa Mwananchi
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amesema uchunguzi kuhusiana afya
ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe bado unaendelea na ni
yeye atakayetangaza matokeo ya kama alipewa sumu au la baada ya
kukamilika huku akiikana ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna, Robert Manumba.
Hii ni mara ya
kwanza kwa Nahodha kutoa tamko hilo tangu kuibuka kwa mjadala kuhusu
afya ya Dk Mwakyembe hasa baada ya DCI Manumba kuutangazia umma kwamba
ripoti kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaonyesha kuwa Naibu
Waziri huyo hakulishwa sumu, kauli ambayo ilipingwa na Waziri mwenye
dhamana ya Afya, Dk Haji Mponda na Dk Mwakyembe mwenyewe.
Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Nahodha alisema uchunguzi kuhusu afya ya Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na hauwezi kufanyika ndani ya wiki mbili au mwezi.
“Ninachosema ni kwamba uchunguzi nilioutangaza bado unaendelea,” alisema na kuongeza: Sasa mimi nimetangaza matokeo ya uchunguzi? Mimi ndiyo Waziri nasema uchunguzi bado unaendelea na mimi ndiyo nitatangaza hitimisho la jambo hilo.”
Alisema suala la Dk Mwakyembe ni zito na siyo la mtu kukurupuka kwani linagusa hisia za watu na kutahadharisha baadhi ya watu wanaojaribu kulifanya jepesi wanachezea kitu hatari.

“Ndiyo maana nasema ni jambo
linalohitaji weledi wa hali ya juu katika kulichunguza. Ni jambo zito la
kisayansi, naomba nipewe muda ili uchunguzi nilioagiza ufanyike kwa
kina. Nasisitiza ni jambo linalohitaji weledi wa kisayansi.”
Waziri Nahodha alisema uchunguzi huo unafanyika kwa kuhusisha jopo la wataalamu wa sayansi hivyo kuwataka Watanzania kutambua kwamba uchunguzi huo unaendelea na ni vigumu kutamka utakamilika lini.
Waziri Nahodha alisema uchunguzi huo unafanyika kwa kuhusisha jopo la wataalamu wa sayansi hivyo kuwataka Watanzania kutambua kwamba uchunguzi huo unaendelea na ni vigumu kutamka utakamilika lini.
Kuhusu ripoti ya DCI
Alipoulizwa ni kwa nini asimchukulie DCI Manumba hatua kwa kutoa tamko wakati uchunguzi alioagiza haujakamilika alisema: “Ndiyo maana nasema, uchunguzi wa suala hili unaendelea. Sasa hatima yote hayo unayozungumza nasema nipeni muda.”
Alipoulizwa ni wapi DCI Manumba alipata
ripoti ya Dk Mwakyembe wakati mgonjwa mwenyewe na Waziri wa Afya
wameikana, alijibu: “Sasa, hilo ni vyema ukamtafuta yeye mwenyewe DCI
aseme. Mtafute aseme yeye na Waziri wa Afya, hao watu wawili wanaweza
kuzungumzia ripoti hiyo, lakini mimi nasema uchunguzi wa jambo hili la
Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na bado unaendelea.”
Alisema
alichokisema DCI Manumba kinaweza kuwa na msingi ambao anaujua mwenyewe
hivyo, ni vyema akaulizwa yeye kuhusu undani wa ripoti yake huku
akisisitiza: "Mimi ninavyoliangalia jambo hili la Dk Mwakyembe
linahitaji umakini wa hali ya juu katika kulishughulikia. Hilo la DCI
mtafute mwenyewe akueleze.”
Nahodha pia hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani hata pale alipoulizwa ikiwa haoni kwamba kukanwa kwa kiwango hicho kikubwa kwa ripoti ya DCI Manumba kunawafanya wananchi waanze kutilia shaka utendaji kazi wa jeshi la polisi.

Hata
hivyo, alipoulizwa jana kuhusu kukanwa kwa ripoti yake na mawaziri,
akiwemo wa Mambo ya Ndani ambayo ndiyo wizara mama inayosimamia Jeshi la
Polisi, DCI Manumba alisema kimsingi hawezi kujibizana na waziri yeyote
kwani kufanya hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu katika utumishi wa
umma.
Alisema alichokifanya ni kuandaa jalada ambalo tayari liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye kwa mamlaka na utaalamu wake wa kisheria, ataamua cha kufanya baada ya kulipitia.
Alisema alichokifanya ni kuandaa jalada ambalo tayari liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye kwa mamlaka na utaalamu wake wa kisheria, ataamua cha kufanya baada ya kulipitia.
“Siwezi
kujibizana na waziri wangu au waziri yeyote. Kama amesema uniulize mimi,
ninachoweza kusema ni kwamba tayari nimeandaa jalada liko kwa DPP. Sasa
nikianza kuzungumza hili au lile itakua haina maana watu watasema
nimeanza kujitetea,” alisema.
DCI, Dk Mwakyembe na Dk Mponda
DCI, Dk Mwakyembe na Dk Mponda
Akizungumza
na waandishi wiki mbili zilizopita, DCI Manumba alisema: “Ukweli kuhusu
kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali
aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa
hakuna sumu.”
“Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya jambo hilo, kwa sasa litashughulikiwa kwa kufuata misingi ya kisheria,” alisema Manumba.
Hata
hivyo, siku moja baada ya kauli hiyo ya DCI Manumba, Dk Mwakyembe
alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema: "Napata tabu kuamini kama
DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au
walisoma taarifa ‘nyingine’ na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au
‘walisomewa!’
“Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa
waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye taarifa
halisi ya Hospitali ya Apollo inayotamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone
marrow (uboho) kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa
wanahangaikia kukijua, kukidhibiti au kukiondoa huku vyombo vyetu vya
dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala
aibu: “Hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu.”
Dk Mwakyembe pia
alitoa sababu kuu tatu za kupinga ripoti ya DCI Manumba: “Kwanza kwa
kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini
chake, unaoendelea katika Hospitali ya Apollo, India ambako bado
sijahitimisha matibabu yangu, pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza
bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa ‘sikunyweshwa
sumu’ wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata
kwa kugusishwa tu.
Tatu ni kitendo cha Polisi kujiingiza kwenye
suala ambalo kwa takriban mwaka mzima sasa, halijawahi kuwa na dhamira
ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia
magazetini.
Januari 19, mwaka huu gazeti hili pia lilifanya
mahojiano maalumu na Waziri Mponda ambaye naye alisema kwa utaratibu,
ripoti ya daktari ni ya mgonjwa... “Sisi hatujaandika ripoti, muulizeni
DCI Manumba awape ufafanuzi.”
Alisema wanaoweza kuzungumzia
maradhi ya Dk Mwakyembe ni familia yake au yeye mwenyewe kwani ndiye
mwenye ripoti. Lakini wizara haiwezi kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment