Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar
Meli
ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH ikiingia katika
Bandari ya Zanzibar ikitokea Oman ikiwa na Lengo la kuimarisha umoja
Amani na Upendo,ikiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi Dkt,Mohammed Bin
Hamed Al Rumhi wa Serikali ya Oman.
Meli
ya iliyobeba ujumbe kutoka Oman ijulikanayo kwa jina la Fulk Al Salamah
ikiwasili katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa na ujumbe wa watu
takribani 350 kutoka Oman.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussen Mwinyi akimlaki
Waziri wa Mafuta na Gesi toka Oman Dkt. Mohamed Hamed Al-
Rumhi ambaye ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman
uliowasili na meli ya mfalme ya Fulk Al Salamah katika bandari ya Dar es
Salaam leo.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo na
Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi walipokutana katika
hafla ya mapokezi ya meli iliyobeba ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman
uliowasili katika bandari ya Dar es Salaam leo. Katikati ni
Mfanyabiashara wa Tanzania Seif A. Seif.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussen Mwinyi akiwa na
kiongozi wa ujumbe kutoka Oman Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt.
Mohammed Hamed Al-Rumhi wakitazama ngoma toka kwa moja ya kikundi cha
watumbuizaji mara baada ya meli ya Fulk Al Salamah ikiwa na ujumbe wa
watu 350 kutoka kwa mfalme wa Oman kutia nanga katika bandari ya Dar es
Salaam leo. Picha na: Frank Shija - MAELEZO
Meli
ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’
iliyofika Zanzibar Oktoba 12, 2017, imeng’oa nanga leo mchana kuelekea
Dar es Salaam kuendelea na safari yake ya kusambaza ujumbe wa ‘Amani na
upendo’ duniani.
Taarifa
kutoka ubalozi mdogo wa Oman zimeeleza kuwa, meli hiyo itakaa Dar es
Salaam kwa siku nne kabla kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo
hayo.
Akizungumza
baada ya kuagana na ujumbe wa meli hiyo bandarini Zanzibar, Balozi
Mdogo wa Oman Dk. Al Habsi, ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzbar
chini ya Rais wake Dk. Ali Mohamed Shein na wananchi wote kwa mapokezi
mazuri na ukarimu mkubwa waliouonesha kwa ndugu zao wa Oman.
Ameomba
hali hiyo iendelee, akisema mahaba na ukarimu ndiyo mambo
yanayowafungamanisha Wazanzibari na Waomani ambao kihistoria ni ndugu wa
miaka mingi.
No comments:
Post a Comment