TOSAMAGANGA ALUMNI ASSOCIATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA ZAIDI YA SH MILION MOJA LAKI SITA KATIKA HOSPITALI YA TOSAMAGANGA
Na Fredy Mgunda,Iringa
Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu
kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wametoa msaada wa mashuka
sabini na tano na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 1,672,500 katika
hospitali ya Tosamaganga iliyopo katika katta ya kalenga mkoani Iringa
kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya afya ikizingatiwa kuwa wengi
wao waliwahi kutibiwa hapo wakati wanasoma.
akizungumza
wakati wa hafla ya kukadhi msaada huo mwenyekiti wa kamati ya
Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha
(ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi alisema kuwa
walijipanga kuja kutoa msaada huu kwa kuwa wangi wao walikuwa wanatibiwa
katika hospital hiyo wakati wakiwa masomoni miaka mingi iliyopita.
“Leo
hii tunaafya njema kwa ajili tulitibiwa vizuri kipindi tulivyokuwa
tunaumwa na ilitusaidia kufanya vizuri masomo yetu na ndio maana leo hii
tupo hapa bila kupata huduma iliyobora nafikiri wengi wetu tusinge kuwa
hapa” alisema Mbilinyi
Mbilinyi
alisema kuwa wamechangisha kidogo walichopata wameamua kununua vifaa
hivyo ambavyo wanafikiri vitakuwa na msaada kwa wagonjwa waliopo
hospitalini hapo.
“Hiki
kidogo tu lakini tunajua kwa namna moja au nyingine vinaweza kuwasaidia
wagonjwa na kuwapunguzia mzigo uongozi wa hospitali yetu pendwa ambayo
imekuwa ikitutibu kwa muda mrefu sana kipindi tukiwa masomoni katika
sekondari ya Tosamaganga” alisema Mbilinyi
Dr
Steven Biginagwa ni daktari bingwa wa magonjwa ya watoto na mtafiti wa
ugonjwa wa malaria alisema kuwa hospital hiyo iliokoa maisha yake kwa
kupata huduma bora kwani alikuwa na ugonjwa wa utumbo kujifunga lakini
madaktari waliokoa maisha yangu hadi hii leo.
“Mimi
nililazwa hapa mwezi wa kwaza na mwezi wa pili wa masomo nilipata
matatizo ya huo ugonjwa lakini nashukuru mungu kuwawezesha wahudumu wote
wa hii hospital kunitibu na kuokoa maisha yangu hadi leo nipo na afya
yangu njema na mfanyakazi niliajiliwa hivyo bila kuwepo kwa hospital hii
sijui leo hii ningekuwa wapi” alisema Dr Biginagwa
Dr
Biginagwa alisema kuwa licha ya kumaliza masomo yake lakini mitihani
mine ya mwisho alifanyia hodini akiwa amelazwa kutokana na ugonjwa
aliokuwa nao na madaktari walimsaidia kupata huduma bora ndio maana
alifanya vizuri mitihani kwenye mitihani na kufaulu vizuri.
“Kwa
miaka yangu vyote miwili nimekuwa nikishinda sana hapa hospitalini
lakini mungu alisaidia nikamaliza masomo yangu na nafikiri kutokana na
hudumu nilikuwa napewa hapa ndio iliyonipelekea kwenda kusomea udaktari
na ndio maana hadi leo hii mimi ni daktari bingwa wa magonjwa ya watoto”
alisema Dr Biginagwa
Kwa
upande wake mkurugenzi mtendaji wa TASAF Ladslausi Mwamanga aliwaomba
wananchi popote walipo hapa nchi kukumbuka kutoa msaada waote katika
hospital ili kuendelea kuboresha sekta ya afya kwa kuwa serikali bila
wadau haiwezi kukamilisha kila kitu yenyewe.
“Unajua
kuwa serikali inamambo mengi ambayo inayaofanya hivyo kukamilisha kila
kitu kwa wakati ni vigumu sana hivyo sasa sisi wadau tuendelee kuisaidia
serikali kwa kile tuchokipata kutoa msaada kwenye sekta hii ya afya
ambayo inachangamoto nyingi sana” alisema Mwamanga
Naye
diwani wa kata ya Kalenga Thobias Kangalawe aliwashukuru wanafunzi hao
waliosoma shule ya Tosamaganga miaka iliyopita kwa niaba ya uongozi wa
hospitali ya Tosamaganga,alisema kuwa ni nadra sana kuona watu
wanakumbuka walikopatia mafanikio na kutoa msaada kama wenu.
Nyinyi
watu wa kipekee kabisa toka nimekuwa kiongozi siajwahi kuona kundi
kubwa lenye kujali wapi walikotoa na kuendelea kutafuta njia mbdala za
kusiadia kutatua changamoto kama nyinyi hivyo hongeni na namuomba mungu
awaongezee pale mlipo punguza” alisema kangalawe.
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu
kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwa wanajadili kitu
walipokuwa kwenye ziara ya kuitembelea shule waliyosoma
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Tosamaganga mkoani Iringa
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwa katika hospital ya Tosamaganga.
No comments:
Post a Comment