DC KASESELA AKESHA KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA SITA USIKU MGODINI NYAKAVANGALA KUOKOA MAITI YA MCHIMBAJI
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika mgodi wa nyakavangala
uliopo katika Kata ya malengamakali Mkoani Iringa wakati wa Juhudi za
kuuokoa mwili wa marehemu viskadi nyenza katika shimo alilosimama Mkuu
huyo wa Wilaya.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akisaiadiana na wachimbaji madini
katika mgodi wa nyakavangala ili kuokoa mwili wa marehemu Nyenza
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipokuwa akiwasili katika mgodi wa
nyakavangala uliopo Kata ya malengamakali Mkoani Iringa.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alilazimika kufanya kazi ya uokoaji
wa maiti ya mchimbaji madini katika mgodi wa Nyakavangala bwana Vaspa
nyenza mkazi wa Itengulinyi Kata ya Ifunda wilaya ya Iringa kwa
takribani masaa kumi na nane
Kasesela
alisema kuwa alianza kazi hiyo majira ya saa mbili asubuhi alipowasili
katika mgodi huyo wa Nyakavangala lakini yeye,waandishi wa habari na
viongozi wengine wa wilaya ya Iringa walijitahidi kuokoa mwili wa
marehemu hadi majira ya saa sita usiku lakini zoezi hilo lilikuwa
likiendelea
"Hadi
saizi tumepiga dua zote lakini hali ngumu sijui nini kinaendelea katika
hili shimo maana waokoaji kila wakiukaribia mwili wa marehemu miamba
laini inavungika na kujaza udongo ndani ya shimo ndio maana mmeniona
naangaika na ndugu wa marehemu kujaribu kusali huku na kule lakini hali
ni ngumu hadi muda huu wa saa tano usiku"alisema Kasesela
Aidha
Kasesela aliwataka ndugu wa marehemu na viongozi mbalimbali kuwa na
subila wakati wanalishugulikia swala la kuokoa mwili wa mpendwa wao kwa
kuwa wameshaukaria mahali ulipo.
"Ungalia
tayari kichwa na kiwiliwili vimeshaonekana kwa hiyo tumebakiza sehemu
ndogo tu naombeni tuwe wavumilivu kwa kuwa tuvumilia toka siku ya
jumapili hadi usiku huu basi tuungane kumuombea mwenzetu ili tutoe mwili
wake ukiwa salama" alisema Kasesela
Haya
yamemkuta mchimbaji mwenzenu hivyo nawataka kuwa makini wakati wa
uchimbaji wa madini katika mgodi huu wa nyakavangala la sivyo mgodi huu
utafungwa sio muda.
Lakini
mwili wa Vaspa Nyenza umepatikana saa 7 na dakika 50 usiku na msafara
kuelekea mortuary umeanza na Mazishi kufanyika Kijiji cha Itengulinyi
Ifunda kesho asubuhi kuanzia saa 3 au 4 hivi
Kwa
upande wake Chief inspector Mayunga Ngele aliwataka wachimbaji wote
kutochimba tena kwenye mashimo yaliyozuiliwa ili kuepusha ajali
mbalimbali hapo mgodini kwa kuwa hata huyo marehemu na wenzake
walishakatwa kuchimba katika shimo hilo ambalo lilikuwa kwenye hali
mbaya ya kuanguka.
"Tamaa
ndio zimemponza huyu marehemu maana tuliwakataza lakini mwenyewe
waliingia kinyemela kwa lengo la kwenda kuchimba kwa wizi kwenye shimo
lilokataliwa ndio maana yamewakuta hayo kama wangekuwa wameusikia
ushauri wetu basi tusingefika hapa tulipo usiku huu "alisema inspector
Ngele
Naye
Thomas masuka mmiliki wa mgodi wa Nyakavangala alimshukuru mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa jitihada zake za kuhakikisha kila
kitu kianda kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na serikali na kuahidi
kuwa gharama za kuuokoa mwili hadi kuufikisha kwako ni kwake na ndugu
hawatalipia pesa yoyote ile.
"Kuanzia
kutokea kwa kifo chake,uokoaji na kuusafirisha mwili wa marehemu huyu
gharama zote nitazilipa mimi kama mmiliki wa mgodi huu kwa mujibu wa
sheria za madini hata angekuwa Mwananchi wa kigoma,Mwanza, Mbeya, Bukoba
na sehemu yoyote ile ndani ya Tanzania basi ni wajibu wangu kuhakikisha
mwili wa marehemu unafika mali pake kwa usalama unaotakiwa" alisema
Masuka
No comments:
Post a Comment