Kamishna wa Madini- Serikali inafanyia kazi vikwazo biashara ya Madini
Kamishna
wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamini Mchwampaka akizungumza jambo
wakati wa Kufunga Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito ya
Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (katikati), Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria Abubakar Bwari (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Abbas Mohamed (wa kwanza kulia) , Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Arusha Peter Pereira ( wa kwanza kushoto ) na Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania Sam Mollel (wa pili kushoto) wakifuatilia kutangazwa kwa washindi wa Mnada wa Madini ya Tanzanite.
Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) akikata kamba maalum katika masunduku yaliyowekwa bahasha za walioomba kununua madini ya Tanzanite kupitia mnada. Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa, (STAMICO) Mhandisi Hamis Komba na kushoto ni Mwakilishi kutoka Kampuni ya TanzaniteOne, Husein Gonga.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kulia) akiangalia zawadi kabla ya kumkabidhi Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Abubakar Bwari (kushoto).
Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Abubakar Bwari (katikati) akiangalia ubora wa Madini ya Tanzanite katika banda la kampuni ya Hadjarat Mining and Gemstone Company Limited. ALiyeshika kifaa cha kupima ubora ni Mkurugrenzi wa Kampuni hiyo.
Baadhi wa washiriki wa Maonesho ya 6 ya Madini ya Vito Arusha wakiwemo wanunuzi na wauzaji wakifuatilia hatua za kumpata mshindi wa Mnada wa Madini ya Tanzanite.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SDK Limited, Susie Kennedy akimwonesha Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Abubakar Bwari bidhaa za madini zinazotengenezwa na kampuni hiyo.
…………………………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Arusha
Wadau wa Madini nchini wametakiwa kujikita katika shughuli za ukataji na usanifu wa madini badala ya kusanifiwa nje ya nchi ili kuwezesha adhma ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda kupitia Sekta ya Madini.
Hayo yalisemwa na Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamini Mchwampaka wakati wa kufunga Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 3-5 Mei,2017.
Aliongeza kuwa, uwepo wa shughuli za ukataji na unga’rishaji wa madini hayo nchini kutawezesha kuyaongezea thamani ikiwemo kupanua wigo wa ajira kupitia sekta ya madini.
” Tanzania ya sasa ni ya Viwanda. Na sisi sekta ya madini tuwe na viwanda vyetu vya kusanifu madini yetu hapa hapa nchini. Kwanza tutayaongezea thamani madini yetu lakini pia tutazalisha ajira kwa wingi,” alisema Mchampaka.
Aidha, Kamishna Mchwampaka aliongeza kuwa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imewasiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya biashara ya Madini nchini ili kuondoa kero ambazo ni kikwazo katika biashara hiyo kwa watanzania.
“Tunataka kuweka mazingira mazuri zaidi kwa wafanyabiashara wa madini wa Tanzania lakini pia tunapenda wafanyabiashara wetu washiriki kwa wingi katika maonesho haya. Ni fursa kubwa ya kibiashara kwao,” alisisitiza Mchwampaka.
Akizungumzia Mnada wa Madini ya Tanzanite uliofanyika tarehe 5 , Mei, alisema kuwa, minada hiyo itaendelea kufanywa mara kwa mara kutokana na mchango wake katika sekta husika kwa kuwa pia inasaidia kupata bei halisi ya madini hayo.
Katika mnada wa Madini ya Tanzanite jumla ya kampuni 48 zilishiriki mnada huo ambapo madini ghafi ya Tanzanite kutoka Kampuni ya TanzaniteOne yenye jumla ya gramu 691,060.33 ziliuzwa katika mnada huo kwa dola za Marekani 3,161,860, sawa na asilimia 100 ya madini yote yaliyowasilishwa kwa mauzo.
Pia, alizungumzia ujumbe wa Serikali ya Nigeria iliyoshiriki Maonesho hayo na kueleza kuwa, ujumbe huo ulifika kwa lengo la kujifunza namna Tanzania inavyoongeza thamani madini yake ikiwemo pia kubadilisha uzoefu na kuongeza kuwa, lengo ni kuifanya Afrika inufaike na rasilimali zake za madini.
Ujumbe wa Serikali ya Nigeria uliongozwa na Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda, Abubakar Bwari aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Abbas Mohamed pamoja na ujumbe wa wafanyabiashara wa Madini kutoka nchini humo.

No comments:
Post a Comment