JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA LUPA AKIWA NA DAWA ZA KULEVYA.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
· MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA SOME WILAYA YA CHUNYA AUAWA KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIVU WA KIMAPENZI.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA LUPA MKOA WA MBEYA AKIWA NA DAWA ZA KULEVYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA KITONGOJI CHA KATAVI – B KILICHOPO WILAYA YA
CHUNYA MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SHIJA PESAMBILI [24]
ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA MIGUUNI NA MKONO WA KUSHOTO NA MTU AITWAYE
MASANJA CHEKA @ DADA.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:30 HUKO
KITONGOJI CHA MANDA - CHINI, KIJIJI NA KATA YA SOME, TARAFA YA KIWANJA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MTUHUMIWA ALIMVAMIA SHIJA PESAMBILI WAKATI AKIWA
AMELALA PEKE YAKE MAKAMBINI NA KISHA KUANZA KUMKATA PANGA SEHEMU ZA
MIGUUNI NA MIKONONI NA KUMJERUHI HALI ILIYOPELEKEA KIFO CHAKE MUDA MFUPI
KABLA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KIPIGO KILICHOTOKANA NA
TUHUMA ZA WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA AMBAYE ALITOROKA BAADA YA
TUKIO KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA MKE WAKE.
UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA MSAKO WA KUMTAFUTA MTUHUMIWA WA
TUKIO HILI.
TAARIFA YA MSAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA
LUPA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA AITWAYE MAGDALENA ODIRO [21] AKIWA
NA DAWA ZA KULEVYA AINA YA BHANGI UZITO WA KILO 01 NA GRAM 700.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.03.2016 MAJIRA YA SAA 17:30
JIONI HUKO KIJIJI NA KATA YA LUPA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO LA MAUAJI AZITOE MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI
ZA KISHERIA. AIDHA KAMANDA MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA
DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment