TBS YATEKETEZA BIDHAA FEKI ZA MAREKANI,CHINA
Katapila
likizikanyagakanyaga kwa lengo la kuziharibu bidhaa mbalimbali zikiwemo
pampasi na dawa za meno zilizopitwa na wakati na zingine zisizo na
ubora katika Dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam. Bidhaa hizo zenye
thamani ya sh. mil. 20, kutoka Marekani na China zilikamatwa na Shirika
la Viwango Tanzania (TBS), katika Bandari ya Dar es Salaam hivi
karibuni. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG).![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVPQ7rOboEJY184nSvkS7a08zCQwTppheg-G1MuvyC9Os5YcJ3q-erjOKkOiAgsb378alISNSo-DTUBZYXOA6tODMlFBCsNwCD9wVIecE-xc9aD5awalbROD1XDPKTfmNt4V1FEvt6fBE/s640/IMG_0812.JPG)
Na Charity James
SHIRIKA
la Viwango Tanzania (TBS), limeteketeza bidhaa hafifu na zilizokwisha
muda wake zenye thamani ya sh. milioni 20 kutoka nchini Marekani na
China.
Akizungumza
wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo,Dar es Salaam jana, Ofisa habari
wa TBS, Roida Andusamile alizitaja bidhaa hizo kuwa ni dawa za meno,
pampas, sabuni za kuogea na wipes.
Alisema
miongoni mwa bidhaa hizo zilikuwa ni kwaajili ya kutoa msaada katika
Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara huku nyingine zikiingizwa
kwaajili ya biashara."Kazi ya kuteketeza bidhaa zenye ubora hafifu ni
endelevu lengo letu ni kuhakikisha tunaepusha madhara kwa watumiaji
ambao wanashindwa kutambua bidhaa hafifu," alisema.
Alisema
bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe za biashara au misaada ni lazima
zipimwe kwa lengo la kuondoa changamoto ya kuwauzia au kugawa zikiwa ni
hafifu au kuisha muda wake.Kwa upande wake, Ofisa Mdhibiti Ubora wa TBS,
Salome Emmanuel alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuakikisha wanaingiza
bidhaa zenye ubora na kuongeza wafanyabiashara ndio walinzi tosha wa
kuhakikisha bidhaa hafifu haziingizwi nchini hivyo ni vizuri wakafuata
sheria kukwepa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment