WAKAZI WA KATA YA NAMAYUNI WAPONGEZA MTANDAO WA SIMU ZA MKONONI WA HALOTEL.
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Halotel ndio mtandao pekee unaotoa huduma za
mawasiliano kwa njia ya Simu za mkononi katika kata ya Namayuni iliyopo
Kilwa Masoko Mkoani Lindi.
Mtandao
huu ndio unawasaidia wakazi wa kata ya Namayuni kuweza kuwasiliana na
ndugu na jamaa wa maeneo hayo na sehemu nyingine kwa njia ya simu ya
mkononi kwa kuwa wamejengewa mnara unao wawezesha kuwasiliana kwa njia
simu za mkononi.
Diwani
wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura
amepongeza mtandao wa simu za mkononi wa Halotel na kusema kuwa
umeisaidia sana jamii ya wakazi wa kata ya Namayuni mkoani humo kutokana
na hapo awali kutokuwepo na mtandao wowote wa simu.
"
Tunawashukuru sana Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kukumbuka kama
kunaviumbe huku na kutuwekea mnara katika kata yetu kwakua kabla ya
mtandao huu tulisafiri na kupanda juu ya vilima ili kutafuta
mtandao(network) ili tuweze kuwasiliana na watu wengine kwa njia ya
simu."
Nao
wakazi wa Kijiji cha Namayuni wamesema kuwa Mtandao huu wa Halotel
"umetusaidi sana katika huduma mbalimbali hasa kutufichia siri katika
mawasiliano kwani tulikuwa tunaenda umbali mrefu kwenda kutafuta
mtandao, kwa sasa tunakaa ndani tuu na tunawasiliana na ndugu na jamaa
bila mtu yoyote kujua kama tumewasilana na nani".
Wafanyakazi wa mtandao wa Halotel wametembelea kata ya Namayuni kwaajili ya Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.
Wafanyakazi wa mtandao wa Halotel wametembelea kata ya Namayuni kwaajili ya Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.
Wanafunzi
wakisoma kupitia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti ya spidi kubwa
walizopewa na kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel katika shule ya
sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mtaalamu
wa masuala ya mtandao wa kampuni ya Halotel, Kilwa Masoko Mkoani
Lindi, Sebastian Inocent akifafanua changamoto mbalimbali zinazo wapata
wakazi wa kijiji cha Namayuni.
Afisa
habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank
Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kilichopo kata
ya Namayuni Kilwa Masoko Mkoani lindi mara baada ya wafanyakazi wa
kampuni hiyo kuwatembelea katika kijijini hapo.
Wakazi wa Kijiji cha Namayuni wakipata maelekezo walipo tembelea kibanda cha kusajili laini jijini hapo.

Kijana akipiga simu kwa ndugu na jamaa wakiwa kijijini hapo.
Baadhi ya waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment