MGODI WA BULYANHULU WATOA ZAIDI YA MILIONI 300 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG'WALE KAMA USHURU WA HUDUMA.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akiwa na wafanyakazi
wengine wa Bulyanhulu Gold Mine wakikabidhi mfano wa hundi kwa kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya Nyang'wale Venance Ngeleuya ,Wengine
wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Ibrahim Marwa
.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akiteta jambo na mkuu wa idara
ya Mahusiano ya Jamii wa Mgodi huo Sara Terri wakati wa hafla ya
kukabidhi hundi.
Madiwani wa halmashauri ya Nyang’wale wakishuhudia makabidhiano ya hundi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyang’wale Venance Ngeleuya akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza na baadhi ya
viongozi na madiwani wa halmashauri ya Nyang’wale (hawapo pichani)wakati
wa kukabidhi hundi kwa halmashauri hiyo.
Viongozi
wa Mgodi wa Bulyanhulu wakiwa kaika picha ya pamoja na Viongozi wa
seriali pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mgodi
wa dhahabu wa Bulyanhulu umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi
Milioni Mia Tatu Thelathini na Nne, Laki Sita na Elfu Themanini na Sita
kwa Halamashauri ya Wilaya ya Nyang’wale.
Fedha
hizo ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%)
ya mapato ghafi ya mgodi huo kwa halmashauri ambapo Bulyanhulu inalipa
kwa halamashauri ya Nyang’wale kutokana na makubaliano ya mwaka jana
kwamba asilimia 35 ya malipo hayo yaende kwa wilaya hiyo na asimia
nyingine kwa Halamashauri ya Msalala ambayo ndiyo mwenyeji wa Mgodi wa
Bulyanhulu kwa asilimia kubwa.
Akipokea
hundi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mheshimiwa Ibrahim Marwa
amesema, “Leo wenzetu wa Mgodi wa Bulyanhulu wamefunga safari kuja
kutuletea hundi ya ushuru wa huduma kwa ajili ya halmashauri ya
Nyangw’ale huo ni mwanzo mzuri, sasa tumepata chanzo kizuri cha mapato
kutoka mgodi wa Bulyanhulu.”
“Lakini
hiyo haitoshi tukijenga mahusiano vizuri watatusaidia zaidi, kuna eneo
lao ambalo kuna wachimbaji wadogo wamevamia eneo hilo na baadhi ya
viongozi wanawatetea, sasa ni lazima tuwe wa kweli kwenye mambo haya ya
msingi, tunataka huku ushuru halafu huku tunataka kutetea wavamizi wa
eneo lao ambalo wanalimiliki kwa leseni halali ya uchimbaji, hivi mtu
akija nyumbani kwako akavamia akasingizia kwamba ana njaa ivi hiyo ni
sababu.”
“Tutachukua hatua za juu ili tuwaondoe wale wachimbaji waliovamia katika kijiji cha mwasabuka wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita”
Akizungumza
baada ya kukabidhi hundi, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham
Crew amesema, “Ninashukuru sana kwa ushirikiano kutoka jamii na wilaya
zinazozunguka mgodi wa Bulyanhulu, nashukuru pia kuona serikali ya awamu
ya nne inahamasisha hapa kazi nafikiri hilo ni jambo zuri tuendelee
kushirikiana ili kwa pamoja tulete maendeleo kwa taifa zima. Ijapokuwa
bei ya dhahabu imeshuka lakini mgodi wetu wa Bulyanhulu bado
umejidhatiti kuhakikisha kuchangia juhudi za maendeleo ya huduma za
maendeleo ya jamii kadiri itakavyowekzekana.
Malipo
ya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi
ya mgodi yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni
zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya
Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement – MDA) baina
ya Serikali na Migodi ikiwemo wa Bulyanhulu, kuhusu ulipaji wa ushuru
wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance
Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000
kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali.
No comments:
Post a Comment