TTCL YAENDELEA KUITAMBULISHA BIDHAA YA 4G-LTE KWA WATEJA.
Baadhi
ya mabango yakiwa yamewekwa na Kamapuni ya TTCL katika maeneo ya
makutano ya barabara Mwenge na Kawe jijini Dar es Salaam kuitambulisha
bidhaa ya 4G-LTE kwa wateja wa jiji la Dar es salaam. Baadhi
ya mabango yakiwa yamewekwa na Kamapuni ya TTCL katika maeneo ya
makutano ya barabara Mwenge na Kawe jijini Dar es Salaam kuitambulisha
bidhaa ya 4G-LTE kwa wateja wa jiji la Dar es salaam.
KAMPUNI ya
Simu Tanzania (TTCL) imeendelea na harakati zake za kimasoko
kutambulisha intaneti yake yenye kasi na bora zaidi ya 4G-LTE kwa wateja
wa jiji la Dar es salaam ili kuwafikia watanzania walio wengi zaidi.
Tangu
kuzinduliwa kwa Huduma hii mwishoni mwa mwezi wa Desemba, 2015, wateja
wengi wamefurahishwa na huduma hii kutokana na ubora wa intaneti,
gharama nafuu ambayo inakidhi mahitaji yao. “Kweli nimeridhishwa na
huduma zao, kwa sasa natumia kifurushi cha Oneconnect ambacho napata
huduma za data ya 4G na ADSL (fixed modem), hii inanisaidia nikiwa
nyumbani na nikirudi nyumbani naendelea kupata huduma kama kawaida kwa
bei moja” alisema mteja, Boazi Kaaya. Pichani
juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza
na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE
kwa wateja anuai. Pichani
juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza
na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE
kwa wateja anuai.
No comments:
Post a Comment