Kilombero Wakabidhiwa jengo la mafunzo na madawati.
Mwakilishi
wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo
Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi jengo
ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa 5.5, Jenga
Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana.
Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto
washio katika mazingira magumu.
Mweka
hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na
vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili
ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu.
Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero.
Mke wa
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Louise
Bainbridge akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilombero,
Muungano, Kantui, Ujirani, Lyahira na Mapinduzi (hapo pichani) wakati
wa hafla ya kukabidhi madawati jana, Kilombero. Katiakti ni Meneja Mkuu
wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mark Roe-Scott na kulia ni meneja
utawala wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Allawi Mdee.
No comments:
Post a Comment