Msama aishukuru Basata
MWENYEKITI
wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama amelishukuru
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa mchango wake wa kufanikisha
maendeleo ya tamasha hilo na sanaa kwa ujumla.
“Tunaishukuru Basata na tunazingatia maelekezo ya Serikali ambayo
ndio muongozo wa kufanikisha maendeleo ya sanaa na wasanii pia,”
alisema Msama.
Msama
alisema yeye na kamati yake wanashukuru kwa kupata kibali kutoka Basata
na wanazingatia maelekezo ya baraza hilo kama ilivyo sheria na taratibu
zinazvyoeleza.
Msama alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi
kwenye tamasha hilo lenye mlengo wa kusaidia jamii yenye uhitaji maalum
kama yatima, walemavu na wajane ambao wanahitaji msaada.
Aidha Msama alisema mbali ya kuhusika na maendeleo ya jamii pia
linafanikisha kuibua vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili ambao
unafikisha ujumbe was neno la Mungu kwa jamii.
“Tamasha la Pasaka malengo yake ni kusaidia jamii yenye uhitaji
maalum pia linaibua vipaji vya waimbaji wa nyimbo za Injili ambavyo
vinatakiwa kutekelezwa kupitia tamasha letu,” alisema Msama.
Msama alimalizia kwa kueleza kauli mbiu ya Tamasha la Tamasa la
Pasaka mwaka huu ni Umoja na Upendo, hudumisha amani katika taifa letu.
No comments:
Post a Comment