Zwelithini alaani mashambulio AK
Mfalme wa kabila la Zulu, Goodwill Zwelithini, ameelezea kama jambo la
aibu mashambulio dhidi ya raia wa mataifa mengine yanayofanyika nchini
Afrika Kusini, ambayo tayari yamesababisha vifo vya watu saba.
Mwaandishi
habari wa BBC mjini Durban mahala ambapo mfalme huyo alitoa matamshi
hayo anasema kuwa hata ingawa anakanusha kuwa amenukuliwa visivyo,
matamshi yake dhidi ya raia wa kigeni imesababisha athari mbaya.
Amesema kuwa umma uliwapigia kelele mabalozi wanaoziwakilisha mataifa yaliyoathirika zikiwezo Msumbiji na Zimbabwe.
Polisi
nchini humo wameakamata washukiwa kadhaa miongoni mwao wanaume watatu
ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya rais mmoja wa Mozambique katika
eneo la Alexandra viungani mwa mji mkuu wa Johannesburg.
Picha kadhaa zimeonyesha Emmanuel Sithole akindungwa kisu huku umati mkubwa ukitizama.
No comments:
Post a Comment