MABASI MAWILI YAGONGANA USO KWA USO LEO MAENEO YA MKATA MKOANI TANGA, WATU ZAIDI YA 10 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA
Basi
la Ngorika likiwa halitamaniki baada ya kugongana uso kwa uso na basi
lingine la Kampuni ya RATCO katika ajali iliyotokea mapema leo kwenye
eneo la Kijiji cha Mbweni, Mkata mkoani Tanga. kwa mujibu wa Ripota wetu
aliopo eneo la tukio,inadaiwa kwamba mpaka sasa ni Watu kumi wamepoteza
maisha katika ajali hiyo, akiwepo Dereva wa Basi la Ratco.Chanzo cha
ajali hiyo hakijafahamika mpaka sasa. Globu ya Jamii inafanya jitihada
za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga kwa maelezo zaidi.
Hivi ndivyo lionekanavyo Basi la Ratco baada ya kupata ajali hiyo leo.
Basi la Ngorika lionekanavyo baada ya ajali hiyo.
Askari Polisi walifika eneo la tukio kwa Wakati ili kuhakikisha usalama unapatikana eneo hilo.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa, na inasikitisha sana.
No comments:
Post a Comment