MGOMO WA MADEREVA WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI WATIKISA NCHI LEO
Madereva
wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, leo
wameingia katika Mgomo wa kutotoa huduma hiyo, kwa kile kinachoelezwa
Madereva hao kutakiwa kurudi vyuoni kwa mafunzo zaidi ya usalama
barabarani.
Hali
ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa
wale waliokuwa wakielekea mikoani, kwani katika Stendi kuu ya Mabasi ya
Ubungo jijini Dar es salaam, hakuna basi hata moja lililoondoka huku
daladala nazo zikiwa hazionekani kabisa vituoni.
Uongozi
wa Madereva hao umeomba kukutana na Uongozi wa Juu Serikalini ili
kulizungumzia swala hilo la kuwataka Madereva hao kurudi mafunzoni,
kwani wao wanadai kuwa kazi wazifanyazo si za kudumu na hivyo
watakaporudi mafunzoni hali ya maisha yao itatetereka.
Mabasi ya Abiria yaendayo Mikoani yakiwa yameegeshwa tu kwenye maeneo yake katika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar.
Wakina
mama hawa wakiwa wamemshikilia Mgonjwa wao waliekuwa wakimsafirisha
kwente mkoani, wakiondoka stendi ya kuu ya Mabasi Ubungo baada kukosa
usafiri kutokana na mgomo wa vyombo hiyo leo.
Huku Ubungo mambo yako namna hii, ni mwendo wa kupiga mguu tu.
Mijadala ikiendelea kwa wadau mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika kituo kikubwa cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar.
Mara
lori likazuiliwa na watu hawa, wakidai kuwa amepakia abiria hivyo
anatakuwa kuwashusha kama anataka kuendelea na safari yake.
No comments:
Post a Comment