CBE YAWAKUMBUKA WAMACHINGA, YAENDESHA UTAFITI KUWASAIDIA KUTAMBULIWA RASMI.
Mkuu
wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema
akitoa ufafanuzi kuhusu utafiti wa wafanyabiashara wadogo wadogo
(wamachinga) unaofanywa na chuo hicho kwa kushirikiana na Shirika la
Wafanyabiashara kutoka nchini Finland (FBMA) kwa lengo la kubaini
fursa za biashara zilizopo , faida, changamoto na mchango wao katika
maendeleo ya taifa pindi watakapoingizwa kwenye mfumo rasmi
unaotambulika kisheria.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Simon Msanjila
akitoa ufafanuzi kuhusu mchango wa utafiti wa shughuli za
wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) unaofanywa na chuo hicho kwa
kushirikiana na Shirika la Wafanyabiashara kutoka nchini Finland
(FBMA) utakavyochangia maendeleo ya sekta ya biashara nchini.
………………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.Dar es salaam.
Chuo
cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kwa kushirikiana na Shirika
la Wafanyabiashara kutoka nchini Finland (FBMA) kinafanya utafiti
wa wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) kwa lengo la kubaini
fursa za biashara zilizopo , faida, changamoto na mchango wao katika
maendeleo ya taifa pindi watakapoingizwa kwenye mfumo rasmi
unaotambulika kisheria.
Akizungumzia
utafiti huo leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel
Mjema amesema kuwa kwa kipindi kirefu wafanyabiashara wadogowadogo
maarufu kama wamachinga wamekuwa katika malumbano na mamlaka za miji na
majiji kote nchini kutokana na kukosa mfumo rasmi unaotambua biashara
zao.
Amesema
chuo chake kwa kuliona jambo hilo kikishirikiana na Shirika la
Wafanyabiashara wa Finland (FBMA) kimeamua kuendesha utafiti huo kuanzia
mwaka 2014 na kuongeza kuwa matokeo ya awali yaliyopatikana ndani ya
mwaka mmoja yamebainisha kuwa jiji la Dar es salaam lina wamachinga
zaidi ya Laki saba (700,000) wanaofanyabiashara zao nje ya mfumo rasmi
unaotambulika kisheria.
No comments:
Post a Comment