KITABU CHA KIGWANGALLA "TANZANIA TUITAKAYO" KUSAMBAZWA NCHI NZIMA
Na Zainul Mzige wa modewjiblog
Mbunge
wa Nzega ambaye amejitokeza kutangaza nia ya kugombea urais nchini
ambaye pia amekuwa mtetezi mkuu wa wananchi wa jimboni kwake kupitia
migodi mbalimbali Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (Mb) ameandika kitabu
kiitwacho "Tanzania tunayoitaka" yakiwa ni mawazo yake binafsi ambacho
anatarajia kukisambaza Tanzania nzima.
Kigwangalla
katika kitabu chake amezungumzia fikra mpya za kuleta mapinduzi ya
kiuchumi na kijamii kutokana na urithi wa rasilimali, utamaduni na
utajiri wa nguvu kazi.
“Kuna mambo misingi minane niliyoipendekeza, ambayo yakifanyiwa kazi tutapata Tanzania Tuitakayo”, amesema Kigwangalla.
"Misingi
hiyo inaunda mfumo mpya wa politikoikonomi unaoitwa Ujamaa wa Kiafrika
wenye Vionjo vya kibepari. Misingi imepewa jina la 'Kigwanomics.',
ameongeza Kigwangalla.
Kitabu
hicho cha "Tanzania tunayoitaka" kwa mujibu wa Kigwangalla mwenyewe
ameeleza kuwa kinapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma
na Iringa huku juhudi zikiendelea kusambaza Tanzania nzima.
No comments:
Post a Comment