Wakazi wa Singida wakipokea vyema CHAMA cha ACT-Wazalendo
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi Manyoni Mjini.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mghwira, akiwahutubia wakazi wa Manyoni Mjini.
Wakazi wa Mji wa Singida wakishangilia viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakati waa mkutano huo jijini humo leo.
Viongozi wakiimba wimbo wa taifa.
Zitto akizungumza na wakazi wa Mji wa Singida leo.
CHAMA
cha ACT-Wazalendo kimesema kinaweza kuunganisha nguvu na vyama vingine
vya upinzani ili kukiondoa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao
ambapo alisema shauku kubwa ya wananchi ni kutaka kujua msimamo wa ACT
Wazalendo katika kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili kufanikisha
malengo ya kuiondoa CCM katika madaraka.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mjini Singida na Kiongozi wa ACT wazalendo Zitto
Kabwe wakati akihutubia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya
msingi ukombozi.
"Tumedhamiria
kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo unaonyonya wananchi.
Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa"alisema na kuongeza
“ACT-
Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili
linathibitishwa na jina letu Alliance na msimamo wetu kuhusu mabadiliko
ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio
ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.
Kiongozi
huyo wa ACT alisema chama hicho hakina tatizo na kipo tayari
kushirikiana na chama chochote kilichokuwa tayari kushirikiana nao
ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Alisema
umoja huo ni lazima uwe na malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye
kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya jamii kwa
wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.
Alikanusha
chama hicho kutoa kauli yeyote dhidi ya UKAWA kama inavyoaminishwa na
baadhi ya watu, bali wameweka wazi kuwa lazima misingi ya kiitikadi na
kifalsafa izingatiwe katika ushirikiano wowote.
No comments:
Post a Comment