COMNETA WAMPONGEZA PROF. MBWETE.
Mwenyekiti wa mtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO FM, Bw.Joseph
Sekiku akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu Huria Tanzania (OUT) ambaye amemaliza muda wake, Prof. Tolly
Mbwete (katikati) iliyoandaliwa na Mtandao wa Redio za Jamii nchini
(COMNETA). Kushoto ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu.
Katibu
wa mtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA), Riziki Leisuya akisoma
risala fupi wakati wa hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria
Tanzania (OUT), Prof. Tolly Mbwete.
Mkuu
wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) ambaye amemaliza muda wake, Prof.
Tolly Mbwete akipokea risala iliyosomwa na Katibu wa mtandao wa Redio
Jamii nchini (COMNETA), Riziki Leisuya wakati wa hafla fupi ya kumuaga
iliyoandaliwa na WanaCOMNETA.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania ambaye amemaliza muda wake, Prof.
Tolly Mbwete (wa pili kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mhariri wa
Sibuka FM, Anita Balingilaki kwa niaba ya Wanamtandao wa Redio Jamii
nchini Tanzania (COMNETA) kama ishara ya kumuaga rasmi wakati wa hafla
fupi iliyoandaliwa na wanamtandao huo ya kumtaki kheri katika majukumu
mapya anayoenda kufanya nchini Addis Ababa.
Kushoto
ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu na Wa pili kulia ni
Mwenyekiti wa mtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO FM, Bw.Joseph
Sekiku akifutiwa na Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Mh. Christopher
Liundi.
Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi akitoa wasifu wa Prof. Tolly Mbwete kwenye hafla hiyo fupi.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) ambaye amemaliza muda wake,
Prof. Tolly Mbwete katika picha ya pamoja na wakufunzi na washiriki wa
warsha ya siku tatu kutathmini mradi wa demokrasia na Amani (DEP) yenye
lengo la kuimarisha ushiriki wa redio za jamii nchini kuelekea uchaguzi
2015 na kura ya maoni kwa wanamtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA)
iliyoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo (UNDP) ambayo imemalizika mwishoni mwa juma katika
ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT)
No comments:
Post a Comment