Header Ads

Waziri Mkuu mstaafu John Malecela, amesema kushabikia wanasiasa wanaojipitisha na kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kabla ya wakati, ni sawa na kupoteza muda, kwani nchi bado in mambo mengi ya maendeleo yanayopaswa kufanywa, kabla ya uchaguzi mkuu.


Waziri Mkuu mstaafu John Malecela  
----
 Waziri Mkuu mstaafu John Malecela, amesema kushabikia wanasiasa wanaojipitisha na kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kabla ya wakati, ni sawa na kupoteza muda, kwani nchi bado in mambo mengi ya maendeleo yanayopaswa kufanywa, kabla ya uchaguzi mkuu.

Malecela ambaye amewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na ni kada wa CCM, alisema hayo jana alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu makada wa chama hicho wanaojipitisha kwa makundi mbalimbali wakitaka waungwe mkono.
“Wananchi wengi wangependa kupata habari za maendeleo kwa ujumla na ni vyema tukaiga mfano wa Uingereza ambako pamoja na kwamba wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu, watu bado wanazungumzia mambo mengine ya maendeleo,” alisema Malecela.
Alihoji,”hapa kwetu ni tofauti, kila siku watu wanazungumzia uchaguzi, kwanini tusiendelee kuzungumzia maendeleo kwanza, halafu masuala haya ya uchaguzi yasubiri muda wake?”
Malecela alisema uchaguzi mkuu hausitishi shughuli zingine za maendeleo, hivyo jamii inapaswa kuendelea kuwajibika katika shughuli hizo badala ya kuweka akili na mawazo yao yote kwenye uchaguzi mkuu ambao hata muda haujafika.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika nyumbani kwake mjini Dodoma mapema mwaka jana Malecela alisema Sekretarieti ya CCM inapaswa kuwachukulia hatua kali makada wanaojipitisha maeneo mbalimbali nchini kwa nia ya kusaka urais, kabla ya chama hicho kupanga muda.
Malecela ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Ushauri la Taifa la CCM, aliwafananisha walioanza mbio za urais kupitia CCM na watu wanaowahi kukimbia kabla ya kipenga kupigwa na kusema hawawezi kupimwa sawa na wale wanaosubiri kuanza rasmi kwa kampeni.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea...

No comments:

Powered by Blogger.