BARABARA KWENDA OLOLOSOKWAN TISHIO KWA MAGARI MAKUBWA
Mkuu
wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (kushoto) akisalimiana na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
aliyemtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kikazi ya siku nne
kwenye kijiji cha Ololosokwani na halmashauri ya Ngorongoro kwa ajili ya
maandalizi ya mradi wa kijiji cha digitali unaoendeshwa na Unesco kwa
kushirikiana na Ki-elektronic ya Samsung unaotarajiwa kuwasili kijijini
hapo mwezi februari ukitokea jijini Dar.
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro.
MKURUGENZI
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues ameonesha mashaka yake
juu ya ubora wa barabara ambazo magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha
digitali Ololosokwan yanaweza kupita.
Alisema
hayo kwenye mazungumzo na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa Lali
wakati alipomtembelea ofisini kwake. Akiwa katika ofisi za mkuu huyo wa
wilaya kumwelezea shughuli za Unesco katika wilaya yake, Mkurugenzi
Mkazi huyo alipata nafasi ya kuzungumzia haja ya kuboreshwa kwa maaneo
kadha ya barabara kuelekea kijiji cha Olosokwan ili kuyawezesha magari
hayo makubwa kufika kwa urahisi.
Huku
akimuonesha mkuu wa wilaya baadhi ya picha alizopiga akiwa njiani
kukagua njia ya kupita magari hayo na kuangalia maandalizi ya mwisho ya
mradi huo mkubwa na wa kipekee nchini alisema hali ya barabara si nzuri
hata kidogo. Vifaa kwa ajili ya kijiji hicho vipo bandarini tayari na
magari yanayoweza kubeba makontena hayo ni makubwa na barabara za
kuelekea kijiji hicho ni mbaya.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) aliyeambatana na wataalamu wa elimu, afya na mawasiliano pamoja na Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia (hayupo pichani)
No comments:
Post a Comment