Rais Kikwete akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa,Ethiopia

Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya taarifa wakati akiwa kwenye
Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa,Ethiopia leo.Kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika
(kulia) wakikutana na marais wastaafu, Thabo Mbeki wa Afrika ya
Kusini(Kushoto) na Joachim Chissano wa Msumbiji(wapili kushoto) wakati
wa mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa
Afrika unaofanyika Addis Ababa Ethiopia leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Malawi Professa Peter
Mutharika jijini Addis Ababa Ethiopia leo.Viongozi hao wanahudhuria
mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika(Wanne
kushoto), Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano, Rais mstaafu wa
Afrika ya Kusini Thabo Mbeki(kulia) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (kushoto)wakiwa katika picha ya
pamoja muda mfupi baada ya kukutana wakati wa mkutano wa wakuu wan chi
wanachama wa AU unaofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia(picha na Freddy
Maro)
No comments:
Post a Comment