Header Ads

Serikali yaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi


 Baadhi ya nyumba zilizojengwa eneo la Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi.
Picha na Hassan Silayo. 
 Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Meja Josephat Musira akiwaeleza Waandishi wa habari (Hawapo pichani)kuhusu Mradi wa ujenzi wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi ambapo kwa awamu ya kwanza idadi ya nyumba 6064 zinatarajiwa kujengwa na mpaka sasa nyumba 1160 zimeshakamilika kwa ajili ya matumizi, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara hiyo Mhandisi Stephen Mpapasingo.
 Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sehemu ya jiko katika moja ya nyumba hizo.
Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaeleza Waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msemaji wa Wizara hiyo Meja Josephat Musira

Frank Mvungi-Maelezo
Serikali yaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi kote nchini.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Meja Josephat Musira wakati wa  ziara ya waandishi wa habari walipotembelea eneo la Gongo la mboto jijini Dar es salaam ambapo sehemu ya mradi huo inatekelezwa.
“Lengo la ujenzi wa nyumba hizi ni kupunguza tatizo la muda mrefu la uhaba wa nyumba kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na  Jeshi la Kujenga Taifa.”alisema Meja Musira.
Akifafanua Meja  Musira amesema awamu ya kwanza ya mradi huo imeanza ambapo  nyumba 6,064 zitajengwa na kugharimu dola za marekani milioni 300, utekelezaji wake unaendelea vizuri  katika Mkoa wa Dar es salaam na Pwani  tayari jumla ya nyumba 3128 zinajengwa.
Kwa Mkoa wa Dar es salaam Meja Musira amesema nyumba 2,228 zinajengwa katika maeneo ya Lugalo, Gongola mboto, Ukonga, Navy Kigamboni, Ubungo Kibangu, Kunduchi KTC, Mbweni JKT  na Kimbiji.
Akieleza zaidi Meja Musira amesema nyumba 1,160 kwenye maeneo manne ya Lugalo na Gongolamboto umeshakamilika kwa asilimia 100 na ukaguzi na uhakiki umeshafanyika.
Kwa upande wa Mkoa wa Pwani Meja Musira alisema  jumla ya nyumba 840 zinajengwa katika maeneo ya msangani,Nyumbu,Kiluvya,Kisarawe na shule ya mafunzo ya awali Kihangaiko.
Maeneo yanayohusika na mradi huu kwa sasa ni Arusha inatarajiwa kujengwa nyumba (792) Tanga (312) Pemba (320) Morogoro (616) Dodoma (592) Kagera (144) na Kigoma (160).
Kwa upande wake Mhandisi wa Wizara hiyo Bw. Stephen Mpapasingo amesema mradi huo unatekelezwa kwa awamu na  unalenga kuondoa kabisa tataizo la makazi kwa  Maafisa na askari wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na  Jeshi la Kujenga Taifa
Mkandarasi wa mradi huu ni kampuni ya Shaghai Construction (Group) General Company  kutoka China

No comments:

Powered by Blogger.