Header Ads

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MAYAMAYA – MELA-BONGA KM 188.15


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete, Mbunge wa Viti maalum kutoka Chama cha Wananchi CUF, Mbunge wa Simanjiro Cristopher Ole Sendeka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi wengine wa Kitaifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela - Bonga Km 188.15. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Serikali ya Japan kushoto, katikati ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli watano kutoka kulia akicheza ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha Bicha kabla ya uzinduzi rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Salama Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na Mzee maarufu wa Wilaya ya Kondoa Balozi mstaafu Mustapha Nyang’anyi kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge.
Katapila likisafisha sehemu ya Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Taswira: ‘Mkeka mpya’ Barabara ya Bicha- Kondoa mjini inavyoonekana mara baada ya kukamilika kwake.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

No comments:

Powered by Blogger.