BILIONI 1.3 ZATUMIKA KUJENGA MAABARA ZA SAYANSI NA HOSTELI
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka akizungumza
Na Denis Mlowe,Iringa
JUMLA
ya sh. bilioni 1.3 zimetumika katika ujenzi wa maabara za sayansi,
hosteli za wasichana na chumba cha darasa katika shule za sekondari za
Ismani, Nyang’ro na Kalenga zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa mkoani Iringa.
Akizungumza na wahabari hivi karibuni ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Iringa,Pudenciana Kisaka alisema
kuwa halmashauri kupitia idara ya elimu Sekondari imekamilisha maabara
tatu za masomo ya sayansi , chumba cha darasa na hostel katika shule
hizo zilizokuwa zina upungufu wa majengo hayo.
Alisema kuwa maabara moja imejengwa katika shule ya sekondari Ismani na ujenzi wake kukamilika kwa asilimia 100 na inatumika kwa masomo ya Bailojia na imegharimu zaidi ya shilingi milioni 89.
Kisaka
alisema shule ya sekondari Kalenga imejengewa maabara mbili ambazo
zimekamilika kujengwa na zinatumika kwa masomo ya Fizikia na Kemia na
kugharimu shilingi milioni 29.
Aidha
alisema halmashauri hiyo imejenga hostel ya wasichana wa shule ya
sekondari Kalenga ambao umegharimu sh. Milioni 258 mpaka kukamilika na
ujenzi wa chumba kimoja cha darasa shule ya sekondari Nyang’oro uliogharimu sh. Milioni 13.
Kisaka
akizungumzia kuhusu mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano alisema
idara ya elimu imepangiwa jumla ya wanafunzi 2389 wa kidato cha tano
katika shule sita hivyo idadi imeongezeka kutoka 1433 mpaka 2389 sawa na
asilimi 156 ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopokelewa kwa mwaka
2013/2014 walikuwa 1433 sawa na asilimia 93.
No comments:
Post a Comment