JESHI LA POLISI LATOA ONYO KALI KWA WANAOTUMIAJI VIBAYA MITANDAO
MSEMAJI wa
Jeshi la Polisi, Advera Senso akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani), Septemba 3,2014 kuhusu kupiga marufuku watu wanaotumia mitandao kinyume
na taratibu.HABARI/PICHA
NA PHILEMON SOLOMON
======== ====== ======
JESHI la
Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kutuma
ujumbe wa matusi, uchochezi, picha za utupu sanjari na kukashifu viongozi wa
Serikali, dini na watu mashuhuri.
Akizungumza
Dar es Salaam, Septemba 3,2014 Msemaji
wa Polisi, Advera Senso alisema kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na
kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.
"Kumejitokeza
tabia kwa baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii na simu za kiganjani
kinyume na malengo yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za uchochezi,
kashfa,kuchafua viongozi wa Serikali.
"Wengine
wamekuwa wanasambaza picha utupu ambazo hazina maadili, hali ambayo ni kosa la
jina, ingawaje mwingine anaweza hasijue kuwa kufanya hivyo ni kosa lakini
sheria haitamuacha, alisema.
Senso
aliendelea kubainisha kuwa kuvunja kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si sehemu
ya kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, atakabainika kutenda kosa hilo bila
kujali anaifahamu sheria au la, atachukuliwa adhabu kali.
Alisema
oparesheni ya kuwabaini wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakamata
waharifu wa aina hiyo.
Aliongeza
kuwa hatua hiyo pia inawatia hatiani wale wote wanaotumia mitandao kufanya
utapeli na kujipatia kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari na blogs
zinazosambaza picha chafu ambazo ni kinyume na maadili.
"Wapo
baadhi ya watu wanatumia mitandao ya simu kutapeli watu na kujipatia kipato,
hivyo nao ni sehemu ya waharifu wanaotafutwa na jeshi la polisi na yeyote
atayekamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake," alisema.
Hivyo
alisisitiza kuwa Jeshi hilo linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uharifu
huo, na kuwataka wale wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa wengine bali
waufute.
Pia
aliziomba kampuni za simu za mkononi pindi wanapoona ujumbe wa aina hiyo
wasiruhusu uende kwa mwingine ili nao wawe sehemu ya kupambana na uovu huo.
No comments:
Post a Comment