Microsoft Windows Phone 8.1yatambulishwa Tanzania kupitia Lumia 930, Lumia 630 and Lumia 530
Meneja
uzalishaji wa kampuni ya Nokia Afrika Mashariki, Kingori Gitahi akiwaonesha
waandishi wa habari moja kati ya simu tatu zilizozinduliwa.
Meneja
Mawasiliano wa Kampuni ya Nokia Afrika Mashariki, Bi.Lilian Nganda akizungumza
na waandishi wa habari Septemba 3,2014 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi
wa simu mpya ya Nokia aina ya Lumia 530, 630 na 930.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia
tukio la uzinduzi wa simu hizo.
Kati ya
wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.
Miongoni
mwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.HABARI /
PICHA NA PHILEMON SOLOMONI
WAFANYABIASHARA
na watumiaji wengine wa simu za kiganjani wamepata matumaini mapya baada ya
simu nyingine tatu aina ya Nokia Lumia 530, 630 na 930 kuzinduliwa.
Kwa mujibu
wa Meneja uzalishaji wa kampuni ya Nokia Afrika Mashariki, Kingori Gitahi
akizungumza Dar es Salaam, Septemba 3, 2014 wakati wa kuzindua simu hizo alisema zinauwezo
mkubwa kwa matumizi ya mtandao.
"Naamini
kwa wafanyuabiashara na watumiaji wa kawaida watakuwa wamepata fursa nzuri ya
kutumia na kupkea email kwa urahisi sanjari na kuchukua picha za video na
zilizomo katika mitandao kwa wepesi,"alisema.
Pia
aliongeza katika kuhakikisha wanatoa huduma nzuri za uhakika wameshirikiana na
kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Vodacom na Airtel ambao hutoa vifurushi
mitandao kwa wateja watakaonunua simu hizo.
Gitahi
aliongeza kuwa simu hizo zinauwezo wa kupiga picha kwa haraka zaidi na kurekodi
matukio mbaliombali kwa ustadi mkubwa na anaamini watu wengi watakuwa watumiaji
wazuri ili kujiweka katika kiwango cha kimataifa.
No comments:
Post a Comment