Header Ads

SHIRIKA LA NYUMBA TANZANIA (NHC) LAKARABATI SHULE YA HASSANGA JIJINI MBEYA.



 Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas  Kandoro akikata utepe kuzindua ukarabati wa Madarasa manne na Jengo moja la Utawala katika Shule ya Msingi Hasanga uliofanyika leo Uyole Mbeya.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas  Kandoro, viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa Tanzania (NHC), Viongozi wengine wa Serikali na Walimu wa Shule ya Msingi ya Hasanga wakifurahia Baada ya Kuzindua Rasmi ukarabati wa ujenzi huo.
Meza kuu
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akizungumza na wananchi, wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi ya Hasanga katika Sherehe ya kukabidhi Majengo ya Shule hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Mchechu akizungumza jambo wakati wa Sherehe hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigallah King akimkaribisha Mkuu wa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro


Gari la Rais lililoibwa Kenya lapatikana Uganda




Msemaji wa Rais alikana kuwa gari hilo lilikuwa limeibwa

Maafisa wakuu kutoka shirika la polisi wa kimataifa, Interpol amethibitisha kuwa gari la ulinzi wa rais Uhuru Kenyatta lililoibwa mjini Nairobi wiki jana limepatikana nchini Uganda. 



Kwa sasa gari hilo limepelekwa mjini Kampala.



Gari hilo aina ya BMW liliibwa siku ya Jumatano usiku mjini Nairobi. Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na wizi huo.Mkurugenzi wa polisi wa kimataifa Interpol nchini Uganda Assab Kasingye aliambia BBC kuwa gari hilo litarudishwa Nairobi. 



Gari hilo liliibwa na watu waliokuwa wamejihami Jumatano wiki jana. Hata hivyo msemaji wa serikali Manoah Esipisu alikanusha habari hizo akisema kuwa gari lililoibwa halikuwa na ulinzi wa Rais Kenyatta bali lilikuwa gari kuu kuu la polisi. 



Lakini lilikuwa linaendeshwa na afisa wa polisi aliyeripoti kuwa gari hilo ni mmoja ya magari ya ulinzi wa Rais.Afisa huyo wa polisi pia alisemekana kuwa mmoja wa maafisa wa polisi wa ulinzi wa Rais.



Tukio la wizi wa gari hilo, lilisababisha taharuki miongoni mwa maafisa wa ulinzi kwa sababu magari ya ulinzi wa Rais yenyewe yanapaswa kuwa na ulinzi mkali. Takwimu za polisi zinaonyesha kuwa visa vitatu vya wizi wa magari huripotiwa mjini Nairobi kila siku. 



Hiki ni kisa kimoja kati ya vingi vya wizi wa magari ambapo mtu yeyote anaweza kuathirika.

No comments:

Powered by Blogger.