Mkongo wa Taifa wasaidia kushuka kwa gharama za mawasiliano nchini
Msemaji
wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bi. Prisca Ulomi
akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya
mkongo wa Taifa ikiwamo kusaidia kushuka kwa gharama za Mawasiliano
nchini. Kushoto ni Mkurugenzi huduma za mtandao wa TTCL Mhandisi Joram
Lujara.
|
Mratibu
wa Ufundi kutoka Ofisi ya Mkongo wa Taifa Mhandishi Anifa Chingumbe
akiwaonesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) maeneo ambayo mkongo wa
Taifa umepita, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Hassan Silayo) |
Frank Mvungi
Serikali
imesema Mkongo wa Taifa umesaidia kushuka kwa gharama za mawasiliano
kwa watumiaji wa mwisho nchini kutoka sh.147 kwa dakika mwaka 2009 hadi
shilingi 62 kwa dakika mwaka 2013.
Hayo
yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya
Mawsiliano Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi wakati wa mkutano na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua
Bi Prisca amesema kuwa mkongo wa taifa umesaidia pia kushuka kwa
gharama za intaneti kutoka shilingi 36,000 hadi shilingi 9000/Gb kufikia
mwaka 2013.
“Mkongo
wa Taifa umesesaidia kuharakisha usambazaji wa huduma za mawasiliano
katika maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara”alisisitiza bi Ulomi.
Katika
hatua nyingine, Bi Ulomi alisema faida nyingine ya Mkongo ni kuongezeka
kwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uwezo wa kusafirisha
masafa.
Akieleza
kuhusu gharama Bi Prisca amesema gharama za maunganisho ya mawasiliano
ya simu za mkononi kutoka kampuni moja kwenda
nyingine (interconnection fees) ambapo sasa gharama imepungua kutoka
sh. 115 hadi shilingi 34.92 kwa dakika.
Mkongo
wa Taifa umesaidia kuongeza ushirikiano wa kikanda kati ya nchi za
Afrika Mashariki na kati ambapo nchi za Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi,
Uganda, na Kenya ambapo hali hiyo imeongeza fursa za kibiashara na
kukuza uchumi wa nchi.
Kufikia
mwaka 2013 makampuni yafuatayo yalikuwa yameunganishwa na mkongo wa
Taifa ni TTCL, TIGO, Zantel, Airtel, Vodacom, Simbanet na infinity.
No comments:
Post a Comment