"WOMEN WITH ATTITUDE" SINEMA YENYE LADHA YA SHUGHULI KUONYESHWA NGOME KONGWE LEO
Mtanzania
mmoja kati ya wawili walioshirikishwa katika filamu ya "Woman with
Altitude" iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP),
Ashura Kayupayupa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari leo mchana
kwenye hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar. Kushoto ni Mratibu wa
Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na Katikati ni Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
UNAWEZA
kudhani kamba kila aliyefanikiwa amezaliwa na kijiko cha fedha, yaani
amezaliwa katika eneo lenye hali shwari na kitanda chake ni mayai ya
dhahabu, kumbe sivyo kabisa. Hili linajadliwa kwa undani katika sinema iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP), Women with Atitude.
Sinema
hii ambayo inaoneshwa katika ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe
imetengenezwa na watanzania kwa ajili ya kuhamasisha Watanzania kutambua
kwamba maisha ni mkusanyiko wa utatuzi wa migogoro inayowakuta na kwa
kupitia elimu.
Women with Altitude inazunguka katika vitu vingi, lakini cha maana ni wanawake wanaojiamini. Baada
ya kufanikiwa kupanda mlima Everest mwaka 2008, wanawake saba wa Nepal
waliamua kupanda milima mingine nmirefu katika mabara mbalimbali wakiwa
na lengo la kutoa ushawishi kwa wanawake na wasichana duniani kote
kufuatilia mambo ambayo yanaonekana ni magumu na hayawezekani.
Machi
2013,wanawake hao walipata ushosti kutoka kwa wanawake wa Kiafrika wane
akiwemo muigizaji wa Afrika kusini Hlubi Mboya,ambaye anatambulika sana
kwa kuigiza nafasi ya mtu anayeishi na VVU kama Nandipha kwenye
Isidingo kupanda mlima mlima mkubwa wa bara la Afrika, Mlima
Kilimanjaro.
Tofauti ya utamaduni na mazingira kwa wanawake wote 11 ilikuwa pia ni ishara ya matatizo waliyokumbana nayo katika maisha yao. Filamu
hii ya Women with attitude inaonesha matatizo ya wanawake hao 11
waliokuwa wakikumbana nayo katika maisha yao yote, na nafasi ya elimu
katika kuwasaidia kufika pale walipo kwa leo.
Wanawake
hawa wanaonekana wakikabiliana na Mlima Kilimanjaro, wakiangalia maisha
ya wenzao na kuwashawishi katika kutokata tama na badala yake kutumia
changamoto kuleta maisha yenye hadhi ya aina yake.
Ofisa habari wa WFP, Fizza Moloo akizungumza
katika mahojiano alisema kwamba taarifa iliyomo ndani ya sinema hiyo ni
ujumbe tosha kwa vijana na wanawake kuhusu ukweli wa maisha na namna ya
kuyabadili.
Baadhi
ya wasanii na waigizaji filamu wanaohudhuria tamasha la ZIFF 2014
linaloendelea kutimua vumbi kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment