SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) LAKARIBIA MWISHO, WASHIRIKI 60 WACHAGULIWA KUENDELEA NA SHINDANO
Baadhi
ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa katika
mazoezi ya Muswada (script) ambayo walipatiwa kwaajili ya Kuonyesha
uwezo wao katika Shindano la TMT ambalo limeingia leo limeingia hatua ya
tatu ambapo washiriki 60 wamefanikiwa kuingia hatua ya nne ambapo
washindi watano kutoka Kanda ya Pwani watatangazwa leo jioni na
kujinyakulia Kitita cha Shilingi laki Tano kila Mmoja.
Baadhi
ya washiriki wakielekea kwenye Chumba cha Majaji kwaajili ya kuonyesha
uwezo wao mara baada ya kukabidhiwa muswada (script) na kuufanyia
mazoezi.
Washiriki wakisubiria kuingia kwa Majaji mara baada ya kumaliza kuifanya mazoezi Script waliyopewa na majaji.
Mmoja
wa washiriki akihojiwa na Msanii wa Vichekesho Tanzania Joti mara baada
ya kutofanikiwa kuingia hatua inayofuata ya kupata washindi watano
watakaiwakilisha Kanda ya Pwani katika fainali kubwa ambayo mshindi
Mmoja ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni Hamsini
Mshiriki
wa shindano la TMT (katikati) akilia mara baada ya kushindwa kuendelea
na shindano hilo linaltarajiwa kumalizika mapema leo kwa washindi watano
kutangazwa na kukabidhiwa Shilingi laki Tano taslimu.
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam
Hatimaye
shindano la Tanzania Movie Talents linatarajia kumalizika mapema leo
kwa washindi watano Kupatikana na Kutangazwa na Jaji Mkuu wa Shindano
hilo Bw Roy Sarungi na kupewa zawadi za Shilingi laki tano kila mmoja na
baadae kuungana na washindi wengine kutoka Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda
za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini katika kinyanganyiro cha kuwania
kitita cha Shilingi Milioni hamsini ambazo atapewa mshindi mmoja
atakayeibuka katika fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa
nane.
Kanda
ya Pwani ambayo inahusisha Mikoa ya Pwani, Dar Es Salaam na Morogoro
itatoa washindi watano ambao nao watajumuika na washindi wengine ambapo
watakaa nyumba moja na kufundishwa sanaa na walimu wa sanaa kutoka Chuo
Kikuu cha Dar Es Salaam na Bagamoyo na baadae kuanza kushindanishwa na
hatimaye kupatikana kwa Mshindi mmoja ambaye ataondoka na donge nono la
Shilingi Milioni hamsini za Kitanzania.
Na
katika fainali hiyo washiriki kumi bora watakuwa chini ya Kampuni ya
Proin Promotions Limited na watafanya kazi ya pamoja na hatimaye kuuzwa
na kunufaika na kazi hiyo.
Vilevile
Vipindi vya Shindano hili la TMT visharushwa katika Kituo cha Runinga
cha ITV na Jumamosi ijayo kipindi cha Dar Es Salaam kitarusha pia katika
Kituo cha Runinga cha ITV saa 4 Usiku na Marudio ni Kila Jumapili saa
10 Jioni na Jumatano Saa 5 usiku.
Usikose
kutazama Vipindi vya TMT ili kuweza kuwaona washindi wa kanda zote za
Tanzania wakishindana na hatimaye kuweza kuona uwezo wao na kuwapigia
washindi watakaonyesha uwezo na hatimaye kumfanya mshindi aliyekuvutia
kuwa Mshindi wa Shilingi Milioni Hamsini za Kitanzania
No comments:
Post a Comment