Tumetoka Mbali: Wazo La 'Mjengwablog' Lilizaliwa Kwenye Mazungumzo Haya Na Ankal Muhidin Michuzi.
Ankal akiwa na Mdau Maggid Mjengwa.
Ndugu zangu,
Septemba
kumi, 2006 nilikutana na ndugu na kaka yangu Muhidin Issa Michuzi pale
Food World Restaurant, Maktaba Street, Dar es Salaam.
Kaka
Michuzi na mimi tulizungumza kwa kirefu juu ya masuala ya kublogu.
Wakati huo blogu ilikuwa ni kitu kipya sana hapa nyumbani. Na hakika
hapa nyumbani alianza Muhidin Michuzi kuwa na blogu ya habari na picha.
Mimi ni kati ya wachache tuliofuatia kwa hapa nyumbani.
Kwenye
mazungumzo yetu pale Food World, nilimwambia Michuzi niwe nachangia
kwenye Michuzi blog kwa kumtumia picha na habari kutoka vijijini, ni kwa
vile nimekuwa nikiishi Iringa na kufanya kazi za vijijini tangu 2004.
Michuzi
aliniangalia na kusema; " Maggid, mimi nafikiri nawe uwe na blogu yako
mwenyewe yenye kutoa zaidi taswira za maisha ya vijijini".
Michuzi
na mimi tumefahamiana tangu miaka ya 80 mwishoni. Kilichotuunganisha na
Michuzi tangu wakati huo ni picha, kama Michuzi, nami pia nimekuwa na
mapenzi makubwa na picha tangu utotoni.
Michuzi aliufahamu uwezo wangu, na ndio maana akaona bora niongeze nguvu kwa kuanzisha blogu yangu mwenyewe.
Na
ndipo hapo ' Mjengwablog' kama wazo l a ' blogu kama kijiji' likazaliwa,
na Jumanne ya Septemba 19, 2006, ndipo picha ya kwanza na maelezo
iliingizwa kwenye Mjengwablog. Naam, nimeratibu shughuli za '
Mjengwablog' kama ' Kijiji' tangu 2006. Ndio sababu ya kuitwa '
Mwenyekiti'. Ina maana ya ' Mwenyekiti' wa Kijiji cha ' Mjengwablog'!
Na profile picture yangu ya kwanza kwenye Mjengwablog ilikuwa nimetinga shati hilo hilo nililovaa nikiwa na Michuzi ( Pichani).
Hakika,
nyingine ni kumbukumbu muhimu sana katika kuandika historia ya chimbuko
la blogu Tanzania. Kuna umuhimu wa kuweka kumbukumbu hizi katika
maandishi ili yasaidie vizazi vijavyo.
Maggid Mjengwa,
0754 678 252
Maggid Mjengwa,
0754 678 252
No comments:
Post a Comment