WAAJIRI NCHINI KUCHUKULIWA HATUA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU
Mkurugenzi
Msaidizi Urejeshaji Mikopo kutoka
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw.
Robert Kibona akitoa mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu
Serikalini mjini Dodoma leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini wakifatilia mada mjini Dodoma leo.
Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini imepanga
kuwachukulia hatua waajiri wote nchini kwa kushindwa kuwasilisha taarifa za wahitimu wa elimu ya juu wanaodaiwa na
Bodi hiyo.
Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji
Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw. Robert Kibona alipokuwa akitoa mada kuhusu
urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa
Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.
“Mpaka
sasa tumewachukulia hatua jumla ya waajiri watano ambao wameshindwa kuwasilisha
taarifa za watumishi wao wanaodaiwa na
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu” alisema Bw.Robert.
Alisema,
mwajiri atakayeshindwa kutoa taarifa za wahitimu wa elimu ya juu katika Bodi
kwa wakati atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni saba au kutumikia kifungo
kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja. Aidha,Bw.
Robert alisema kuwa mpaka sasa takribani waajiriwa 18 wamefikishwa mahakamani
kwa kosa la kushindwa kurejesha mikopo hiyo.
Bw.Robert
alifafanua kuwa ili kufanikisha zoezi la urejeshaji mikopo kutoka kwa wadaiwa, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatunga
sheria na mifumo mbalimbali ya
kuwadhibiti wadaiwa hao. “Tunatengeneza
sheria ambazo zitawazuia wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kupata hati ya
kusafiria nje ya nchi au kibali cha kusafiri hadi atakapowasiliana na Bodi.”
Pia,alisema
mhitimu atakayeshindwa kulipa mkopo taarifa zake zitatangazwa kwenye vyombo vya
habari na kwenye taasisi za mikopo ili asipate huduma yoyote ya kifedha.
Naye,
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Dk. Veronica
Nyahende amewataka wahitimu wa elimu ya juu nchini kutumia elimu waliyonayo
kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa. Alisema
changamoto ya kurejesha mikopo ni kubwa
kwa upande wa wahitimu wa elimu ya juu ambao hawana kazi ama hawajajiajiri.
“Changamoto
iliyopo ni wahitimu kushindwa kulipa mikopo hiyo kutokana na kuwa na kipato cha
chini ama kukosa ajira.” Alisema
Bodi imeingia mkataba na kampuni zitakazokusanya mikopo kwa walionufaika na
mikopo hiyo na kushindwa kuilipa .
Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu iko katika mchakato wa kuelimisha umma na watendaji
wakuu Serikalini ili kuhakikisha wanawasilisha taarifa za watumishi wao
wanaodaiwa mikopo hiyo.
No comments:
Post a Comment