Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Kigoda aongoza mkutanno wa 99 wa baraza la mawaziri nchini kenya.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), akiwa katika
picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mhe. Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya
mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na
Ulaya katika ukumbi wa Kenyata International Convention Centre hivi karibuni
jijini Nairobi, Kenya. Kushoto kwa Rais Kenyata ni Rais wa Baraza la Mawaziri
wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Mheshimiwa Kyriakos Gerentopoulos. Ujumbe wa
Tanzania ulishirikisha pia Mhe. Janet Mbene (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara (aliyevaa gauni la kijani).
Mheshimiwa
Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara akimshukuru Mhe.
Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa
39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na Ulaya katika ukumbi wa Kenyatta
International Conference Centre jijini Nairobi, Kenya.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), na Rais wa
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika, Carribean na Pacific akiongoza Mkutano wa
99 wa Baraza hilo la Mawaziri. Kushoto kwake ni Mheshimiwa Adan Abdulla
Mohamed, Waziri wa Viwanda wa Jamhuri ya Kenya akifuatilia mkutano huo
uliofanyika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre, Nairobi Kenya.
No comments:
Post a Comment