Picha na Taarifa:Majambazi Yavamia Kituo Cha Kidogo cha Kimanzichana Pwani na Kuua Askari Polisi
Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha
Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema
waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa
na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu
wanaohitaji msaada.
Cha
kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika
kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye
kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30.
Ndipo
walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora
SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41
na kutoweka kusikojulikana.
Askari
Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali
ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa
mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa
kulia.
Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni.
Kwa
mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA
MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo
Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.
Kazi
ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya
ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata
watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa
ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako
kuhusiana na wahusika wa tukio hili.
AMEN
CHANZO:Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment