Header Ads

H.BABA ASHINDWA KUMUAGA TYSON, ASHIKWA NA HOMA KALI

H-Baba alazwa
H-Baba
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamisi Ramadhani Baba, maarufu kama ‘H.Baba‘ ameshindwa kutoa heshima za mwisho kwa  mwili wa marehemu George Tyson ulioagwa katika viwanja vya Leaders Club baada ya kupata homa kali iliyompelekea aanguke ghafla wakati akijiandaa kuelekea msibani na kukimbizwa hospitalini.
Mkali huyo mwenye vipaji lukuki ikiwemo uigizaji aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa hospitalini na dripu mkononi na kisha kuandika ”Naumwa sana nilikuwa najiandaa kwenye kumuaga mwenzetu #tyson nikaskia kizunguzungu nikaanguka apa nipo hosp”. Get Well Soon Bro
H_Baba Tanzania H-Baba 
H.baba akiwa hospitalini na Dripu mkononi

No comments:

Powered by Blogger.