RAIS JAKAYA KIKWETE AMPIGIA PANDE DIAMOND PLATNUMZ
”Wapi
Utapata Rais ambaye atakubali kutoa muda wake wa Thamani ambao
unatafutwa karibu na kila mtu Duniani..akautumia kukusaidia
kukukutanisha na kukuconnect na Mdau mkubwa Duniani katikaa tasnia
uliyopo, ili kuhakikisha tu Unafikia Malengo na Ndoto ya kazi zako”
hayo ni maneno mazito aliyoandika Mwanamuziki Diamond
Platnumz kwenye ukurasa wake wa Instagram akimshukuru Rais Kikwete
ikiwa ni masaa machache tangu mwanamuziki huyo aposti picha akiwa amekaa
meza moja na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Kevin Liles aliyewahi kuwa Rais ya rekodi lebo maarufu Duniani ya Def Jam na
Makamu wa Rais wa The Island Def Jam Music Group iliyowahi kuwatoa
wakali kama vile Jay Z, Snoop, Young Jeezy, usher na wengine kibao.
Wahenga wanasema dalili za mvua ni mawingu na huenda hii
ikawa ni fursa ya kipekee kwa Diamond kuweza kuitambulisha Tanzania
katika anga la muziki wa kimataifa baada ya kukutanishwa na mdau huyo
mkubwa wa muziki aliyeweza kudumu katika gemu kwa kipindi kirefu hasa
ukizingatia kwa sasa Diamond ametajwa kuwania takribani ya Tuzo kubwa
Tano ikiwemo ile ya BET, MTV, KORA na AFRIMMA. All The Best Rais wa
Wasafi. Kwa picha unaweza ukatazama hapo chini.
Pichani ni Diamond Platnumz akiwa amekaa meza moja na mdau Kevin Liles pamoja na Rais Kikwete
No comments:
Post a Comment